ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 7, 2016

ASKOFU TUTU AOMBA KUSAIDIWA KUFA.

Desmond Tutu akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 85
Askofu Desmon Tutu akisherehekea sikukuu yake ya kutimiza umri wa miaka 85.

Askofu mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu amesema katika ujumbe wake wa siku yake ya kuzaliwa katika gazeti la Washington Post kwamba angependelea kusaidiwa kufa atakapo uguua.
Katika ujumbe huo Tutu alisema: Nimejiandaa kufa na nimesema wazi singependelea kuendelea kuishi kwa gharama yoyote.Ningependa kutibiwa na mapenzi na kuruhusiwa kufariki vile nipendavyo.Watu wanaokufa wanapaswa kuwa na haki ya kuchagua vile na lini watakavyokufa.Ninaamini kwamba,mbali na uuguzi uliopo ,chaguo lao linafaa kushirikisha kusaidiwa kufa kwa heshima.
Alitangaza hatua yake ya kuunga mkono wazo hilo baada ya kulipinga 2014.
Habari kwamba Desmond Tutu angependa asaidiwe kufa sio swala la kushangaza nchini Afrika Kusini.
Swala la kusaidiwa kufa limeigawanya nchi hiyo kwa kipindi cha muda sasa.
Mwaka uliopita mahakama kuu katika mji mkuu wa Pretoria iliamuru kwa kumpendelea mgonjwa mmoja aliyekuwa anaugua saratani kupita kiasi, Robin Strasham-Ford ambaye alikuwa ametoa ombi la kusaidiwa kufa.
Alikuwa amesalia na wiki mbili pekee kufariki na alitaka sheria irekebishwe ili asaidiwe kufa bila ya kuwepo kwa kesi.
Sheria ilikuwa wazi,daktari yoyote ambaye angemsaidia mgonjwa kufariki angepewa hukumu ya miaka 14 jela.
Taifa hilo halina sheria ya kusaidiwa kufa,huku katiba ikilinda haki ya kila mmoja ya kuishi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.