Airtel yazindua “Airtel SimuBima” kuwezesha wateja kupata fidia za simu zao nchini.
· Wateja wa mitandao mingine pia wataweza kusajili simu zao na bima hiyo na kulipia kwa Airtel money
· Airtel Simu Bima kufidia simu za wateja wake zilizopotea au kuibwa
Kampuni ya simu za mkononi Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya UAP leo wamezindua huduma kabambe itakayowasaidia wateja wote wanaotumia Simu za Smartphone kuziwekea Bima simu zao na kulipia kupitia huduma ya Airtel Money.
Huduma hiyo mpya nchini kwa watumiaji wa smartphone itajulikana kama “Airtel SimuBima” ambapo itawawezesha wateja wa Airtel pamoja na watumiaji wote wa Smartphone nchini kuepuka hasara pale simu inapopotea au kuibiwa.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbandoalisema “Leo Airtel tumeongeza sababu nyingine kwa wateja wetu kuendelea kufurahia huduma zetu, sasa wateja wote wenye simu orijino za smartphone wataweza kusajiliwa na huduma ya ‘Airtel SimuBima’ ambapo mteja mmoja anataweza kusajili hadi simu mbili katika mfumo huu. Ikitokea mteja ameibiwa simu yake au kuipoteza basi kupitia huduma hii ya ‘Airtel SimuBima’ tutampatia mteja huyo pesa ili aweze kununua simu nyingine atakayotaka na kisha simu iliyopotea itazimwa moja kwa moja isiweze kutumika tena”.
“Mteja wa Airtel ataweza kufaidi huduma ya “Airtel SimuBima” mara baada ya kupakuwa aplikesheni ya simuBima kutoka kwenye Playstore na kusajili taarifa za smartphone yake ikiwemo IMEI namba pamoja na gharama ya simu yake na papohapo atapata ujumbe utakaomwambia gharama ya Bima ya simu hiyo kwa mwaka ambayo ataamua kuilipa yote au kuwa anailipa kwa kila mwezi” aliongeza Mmbando
“Airtel Tanzania tunaamini kuwa ushirika wetu na shirika la bima la UAP kupitia ‘Airtel SimuBima’ utasaidia kuhamasisha watumiaji wa simu za mkononi kununua simu orijino ili waweze kufurahia huduma hii pamoja na huduma zingine za Airtel za kimtandao kama vile Airtel TV, Kujisomea masomo ya VETA –VSOMO kupitia mtandao pamoja na kufaidi aplikesheni mbalimbali za airtel zenye kusaidia wateja katika mambo ya kiuchumi na kijamii” alieleza Mmbando
Kwa upande wake Mkurugenzi wa UAP Bw, Raymond Komanga alisema “tunawahakikishia wateja wote wa Airtel watakaosajili namba zao katika huduma ya Airtel SimuBima kwamba tutawalipa madai yao haraka sana pale wanapopatwa na tatizo la kupoteza simu au kuibiwa simu zilizowekewa Bima ndani ya siku tano tu tokea pale wanapotoa taarifa kituo cha polisi na kutujulisha sisi, tutalipa simu za hadi shilingi milioni moja na laki tano, lakini wateja waelewe kuwa bima yetu haitakuwa ikilipa simu kuvunjika au
Komanga aliendelea kuelezea kuwa “Ikitokea simu ya mteja iliyosajiliwa na “Airtel SimuBima” imepotea au kuibiwa mteja atatakiwa kutoa taarifa mapema sana na kupata taarifa ya polisi kuhusiana na upotevu huo au wizi ili kuweza kukamilisha malipo yake. Swala hili linatakiwa kufanywa na wateja wote waliojisali na kulipia bima ya mwezi au ya mwaka mzima kupitia Airtel SimuBima”
Wateja wa “Airtel SimuBima” wataweza kudai malipo yao kwa kutumia simu nyingine ya smartphone na kuingia katika Aplikesheni ya Airtel SimuBima kisha kufuata maelekezo ya malipo. Vilevile mteja anaweza kutumia kompyuta na kuingia katika ukurasa wa ‘Airtel SimuBima’ na kukamilisha taarifa za madai.
“Ukitaka kulipia huduma hii ya ‘Airtel SimuBima’ piga *150*60# kisha chagua malipo, na uchagueSimuBima, papohapo malipo yatatufikia sisi moja kwa moja”. Bw, Komanga alisema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.