YAMOTO BAND NA MSANII WA ETHIOPIA LIJ MICHAEL KUUNGANA KWENYE COKE STUDIO AFRICA 4
Kundi la Yamoto Band lipo jijini Nairobi, Kenya kuiwakilisha Tanzania kwenye kipindi maarufu cha Coke Studio Africa. Wataonekana kwa mara ya kwanza kwenye show hiyo mwaka huu kwa kuungana na msanii wa Ethiopia, Lij Michael, aliyejipatia umaarufu kwa wimbo ‘Zaraye yehun nege’ ambaye pia anashiriki kwa mara ya kwanza kwenye msimu wa nne wa Coke Studio Africa.
Wasanii hao wanatarajiwa kujumuisha ladha za Bongo na vile vya hip hop ya Ethiopia, huku wimbo wao ukitayarishwa na producer wa Ufaransa, DSK (asili yake ni Ivory Coast).
Akiongelea kushiriki kwa mara ya kwanza, msanii wa kundi hilo, Enock Bella alisema, “Naishukuru Coke Studio Africa kwa kutuamini na kutupa fursa kushiriki kwenye kipindi kuonesha uwezo wetu katika hatua hii ya mwanzo ya muziki wetu. Tunafurahia kufanya kazi na Lij Michael na tunategemea kuchanganya muziki wa Bongo Flava na muziki kutoka Ethiopia,” na kuongeza, “Studio na utayarishaji upo katika ukubwa ambao hatujawahi kuuona kabla na tuna hamu kubwa.”
Lij Michael pia aliisifia Coke Studio Africa akidai kuwa mabadilishano kati ya Yamoto Band na yeye ni ya kupendeza. Akiweka wazi kile mashabiki wanapaswa kungojea, alisema “Mtayarishaji wa mdundo DSK alitupa ladha kama za mdundo wa asili ya Tanzania na wakati huo huo nimepata mdundo halisi wa nchi yangu ya Ethiopia. Pindi show ikianza, tazamieni tumbuizo la uhakika – itakuwa ya moto.”
Yamoto Band na Lij Michael watakuwa wenyeji kwenye ukurasa wa Facebook wa Coca-Cola kuanzia saa nane mchana Alhamis hii, Septemba 1. Usikose kutazama kuwaona live. Watajibu pia maswali yako kuhusu safari zao kimuziki. Andika swali lako kupitia @CocaColaAfrica na weka hashtags: #AskYamotoBand #AskLijMichael #CokeStudioAfrica
DSK ni mongoni mwa watayarishaji wa muziki Afrika kwenye kipindi cha msimu huu na amepewa jukumu ya kuzifanyia kazi mchanganyiko wa muziki uliochaguliwa kutoka zaidi ya nchi kumi na mbili. Wengine ni pamoja na Madtraxx (Kenya), Bushingtone (Uganda), Masterkraft (Nigeria), Chopstix (Nigeria) na Maphorisa (Afrika Kusini).
DOKEZI KWA WAHARIRI
Coke Studio Africa ni kipindi kisicho cha mashindano kinachowakusanya pamoja na kuangaza vipaji mbalimbali vya Afrika. Pamoja na Kenya, Uganda, Tanzania, Nigeria na Msumbiji, msimu wa nne sasa unajumuisha nchi za Ethiopia, Togo, Ghana, Cameroon na Ivory Coast. Kipindi huwapa wasanii kutoka kwenye mahadhi yote fursa ya kufanya kazi na na watayarishaji bora na wenye vipaji wa nyumbani na wa kimataifa.
Yamoto Band inaundwa na wasanii wanne wenye vipaji wa Tanzania, Dogo Aslay, Maromboso, Enock Bella and Beka 1. Ni miongoni mwa makundi ya Afrika yanayokua haraka Afrika na wanapendwa kwa nyimbo zao zikiwemo “Niseme”, ”Yamoto” na “Nitajuta”. Mtindo wa uimbaji wao umefanya wawe na mashakibi wengi Tanzania na nje. Wakati wakiendeela kufanya mambo makubwa kwenye tasnia ya muziki, kundi hilo linaendelea kutayarisha nyimbo zenye ubora.
Nitakupwelepeta: https://www.youtube.com/watch? v=k7uMsGcNqmA
Lij Michael aka Faf ni rapper mkongwe wa muziki wa hip hop nchini Ethiopia. Akijulikana kwa aina yake ya kipee ya muziki na uwezo mkubwa wa kutumbuiza, anajisifia mwenyewe kuwa muasisi wa tasnia ya burudani kwao. Akichanganya ladha za Ethiopia na hip hop, Lij anawakilisha kizazi kipya cha muziki wa Ethiopia.
Alrada Larada: https://www.youtube.com/watch? v=fogPqlR2d_I
Mfollow @skytanzania kwenye Instagram au soma makala zake mbalimbali kupitia bongo5.com
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.