Mbio zilizokuwa gumzo zaidi ni zile za kilomita 21 ambapo washiriki toka nchi za Afrika Mashariki na kati, Kenya, Uganda, Rwanda, Zambia, Burundi na wenyeji Tanzania walijitokeza na kushiriki.
Michuanao hiyo ilikuwa imegawanyika katika
makundi mbalimbali ya Km 21,5,3 na 2 ambapo washindi wote wa kwanza upande wa
wanaume na wanawake ni washiriki kutoka Tanzania upande wa Km
21 ni Chacha Boy na Thailun Abdul wakijinyakulia sh milioni moja na
nusu kwa kila moja ikiwa na medali na Cheti.
Aidha kwa upande wa
kilomita 5 kwa wanawake na wanaume walijinyakulia zawadi
ya sh laki tisa na medali na Cheti ni Barnad Samike naHelena Bahati na Km 3,
Germia Kinshuli na Chirstina Urio na Km 2 ni Winefrida Mathayo naSamsoni
paul.
Naye meneja wa NSSF Hamisi Fakii amesema ili Tanzania ipate mafanikio katika sekta ya mchezo wa riadha wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki michuano hiyo na kuipa msisimko nalo shirika lake likiahidi kujitokeza kila mwaka kudhamini mashindano hayo ili kuhakikisha kukuwa kwa michezo nchini
ikiwa ni moja wapo ya ajira kwa vijana na wazee.
GSENGO BLOG ikizungumza na washindi hao
walisema wanamshukuru mwenyezi mungu kwa kuibuka washindi na kuipeperusha vyema
Tanzania kwani miaka ya nyuma washiriki wa nchi zingine ndio walikuwa
wanajinyakulia ushindi hivyo jitihada zao na mazoezi ndivyo vilivyowafanya kuwa
washindi.
Walisema maandalizi ya mwaka huu yalikuwa
mazuri japo kuwa walikabiliwa na changamoto ya magari kwa
sababu mpangilio haukuwa mzuri walipokuwa wakimbia wanapishana na
magari kitu ambacho ni hatari kwa maisha yao pia waliwataka watanzania kufanya
mazoezi kwani ni msingi mzuri kwa maisha yao utakao saidia
kupeperusha Bendera ya Taifa na kuwafanya nchi zingine waone Tanzania
inaweza kuliko wao.
Naye mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella
ambaye alikuwa mmoja wa washiriki aliwashukuru wadhamini walioandaa
mashindano hayo NSSF, NMB, Mwanza hotel, FABEC, Real Pr Solution, Puma Energy,
TIPER na Friekdin Conservation Fund kwa kuona umuhimu na kujali thamani ya
michezo pia aliwataka waendelee kujitoa na kudhamini na vitu vingine ili kuleta
maendeleo zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.