ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 15, 2016

UKOSEFU WA WAKUNGA CHANZO CHA VIFO VYA MAMA NA MTOTO

Na Annastazia Maginga, Mwanza. 
MAZINGIRA duni ya kutolea huduma za afya umekuwa chanzo cha wanawake 145 Mkoni Mwanza kupoteza maisha wakati wakijifungua. 

 Hali hiyo imesababishwa na ukosefu wa wakunga na watoa huduma ya afya kwenye vituo mbalimbali hatua inayopelekea kushindwa kunusuru maisha ya mama na mtoto. 

 Kaimu mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt Silas Wambura wakati akizungumza na wadau wa afya kutoka mikoa nane ambapo walikutana ili kujadili namna ya kupunguza vifo vya mama na mtoto hasa kwenye maeneo ya vijijini ambako tatizo ni kubwa.

 “Vifo 130 vilitokea kwenye vituo vya Afya pamoja na hosptali wakati vifo 15 vikiwa vimetokea nyumbani kwa hiyo tunahitaji kusadia ili kuokoa maisha ya mama na mtoto” amesema Wambura. 

 Mratibu wa taifa wa chama cha wakunga nchini (TAMA)Martha Rimoy amesma kuwa upungufu wa wakunga unatokana na wanafunzi wanaohitimu kwenye vyuo mbalimbali kuwa wachache ukilinganisha na idadi ya vituo vya afya. 

 “Idadi ya Vituo ni kubwa ukilinganisha na idadi ya wanafunzi wanaomaliza kwenye vyuo vya uuguzi na ukunga hivyo mzigo huwa mkubwa katika kuukabili lakini tunajitahidi kadri ya uwezo wetu”Martha. Mwisho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.