NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
VIJANA zaidi ya 175 wanaoishi katika mazingira magumu kutoka kata ya Visiga Wilayani Kibaha Mkoani Pwani wamepatiwa mafunzo ya ufundi stadi pamoja na ujasiriamali lengo ikiwa ni kuweza kuondokana na tatizo sugu la ajira na kuachana na kuwa tegemezi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake waliofanya ziara ya siku moja kwa ajili ya kujionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na vijana hao, Afisa mtendaji wa kata Loisia Nyawa alisema kwamba vijana hao wameanza kunufaika baada ya kukamilika kwa maradi wa kuwawezesha vijana kiuchumi ilikuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
Loisia alisema kwamba mradi huo ambao upo chini ya shirika lisolokuwa la kiserikali la Plan international umeweza kuwa ni mkombozi mkubwa kutokana na kuweza kuwapatia mafunzo katika fani mbali mbali ambayo yameweza kuwapa fursa ya kujiajiri wao wenyewe na kuendelea kuendesha shughuli zao.
“Mradi huu wa Plan International wa kuwawezesha vijana vijana kiuchumi katika kata ya ngu ya Visiga uwemewa kuwa ni moja ya mkombozi mkubwa sana, kwani baada ya vijana hawa kupatiwa mafunzo mbali mbali wameweza kuelemika na kwa sasa tunaona mafanikio makubwa ambayo yameweza kuwabadilisha kimaisha,”alisema Mtendaji.
Aidha alifafanua kuwa hapo awali kabla ya kuanza kwa maradi huo kulikuwa na makundi ya vijana wengi ambao walikuwa wanashinda kwenye vijiwe kutwa nzima bila ya kuwa na kazi yoyete ya kufanya lakini kwa sasa wameweza kunufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na mafunzo waliyopatiwa.
Pia katika hatua nyingine aliwaomba vijana wengine kuachana na tabia ya kuwa tegemezi na badala yake wahakikishe wanatumia fursa za kijiendeleza zaidi kupitia mradi huo wa plan ili kuweza kupunguza idadi ya vijana ambao wapo mitaani bila ya kuwa na ajira.
Kwa upande wao baadhi ya vijana ambao wamenufaika na mradi huo akiwemo Simba Simba,Rajabu Kilanga, pamoja na George Mgoli walisema kwamba baada ya kumaliza mafunzo kutoka chuo cha Veta kwa sasa wameweza kupiga hatua kubwa kutokana na kujiajiri wao wenyewe na kuendesha maisha yao wenyewe bila ya kuwa tegemezi.
Walisema kwamba awali kabla ya kuanza kwa maradi huo masiha yao yalikuwa magumu kutokana na kukosa ajira lakini baada ya kumaliza mafunzo yao wameweza kupata fursa nyingi za kujiajiri na wengine kuajiriwa katika maeneo mbali mbali.
“Sisi tunapenda kutoa pongezi zetu za dhati kwa kuwepo kwa mradi huu ambao upo chini ya shirika la Plan International pamoja na wafadhili wengine kwa kweli wameweza kutusaidia sana kwa kutupeleka chuo cha Veta na kujifunza fani za aina mbali mbali na hii kwetu ni hatua kubwa ya kutufungulia milango ya ajira na kuweza kukuza uchumi na kuleta maendeleo,”walisema.
MRADI huo wa YEE upo chini ya Plan International na umefadhiliwa na jumuiya ya umoja wa nchi za Ulaya ambapo umeweza kuwasaidia vijana zaidi 175 ambao wamehitimu katika fani mbali mbali ikiwemo udereva, ufundi magari, ushonaji ,fundi umeme, ufundi ujenzi,upinshi pamoja na upambaji katika chuo cha ufundi stadi VETA Mkoa wa Pwani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.