Wachezaji wa
timu ya New Generation wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa
baada ya kuifunga Women Fighter 2-1 kwenye fainali za michuano ya Airtel Rising
Stars Zanzibar, zilizochezwa kwenye uwanja wa Fuoni Alhamisi 25 Agosti 2016
Naodha wa timu ya
Mbaspo Academy Mbeya, Biva Steven akipokea kikombe kutoka kwa mgeni rasmi Katibu
Tawala wa mkoa huo Alone Mbinga baada ya timu yake kuifunga Uyole Alois Academy
Penati 4-3 katika mchezo wa fainali ya
Airtel Rising stars ngazi ya mkoa uli0pigwa katika dimba la uwanja Sokoine
juzi.
Wachezaji wa
Mbaspo wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe cha ubingwa wa Airtel Rising
Stars mkoa wa Mbeya juzi.
New Generation,
Mbaspo mabingwa Airtel Rising Stars
TIMU ya wasichana ya New Generation imefanikiwa kutwaa ubingwa wa
michuano ya Airtel Rising Star, Zanzibar, baada ya kuifunga Women
Fighter kwa mabao 2-1 katika fainali iliyochezwa visiwani humo jana.
Mchezo huo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa Fuoni nje kidogo ya mji
wa Zanzibar na kuvuta hisia za mashibiki wengi wa soka wanawake na wanaume,
hasa kwa vile timu hizo zina upinzani wa jadi.
Mabao ya New Generation yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza ambapo
bao la kwanza lilifungwa na Warda Mwinyi katika dakika ya 10 wakati bao la pili
lilifungwa mnamo dakika ya 16 wakati bao la kufutia machozi la Women Fighter
lilifungwa na Khadija Hassan dakika ya 27.
Akizungumza wakati wa kukabidhi kombe kwa washindi afisa habari wa chama
cha soka Zanzibar ZFA Ali Bakari Cheupe kwa niaba ya rais wa chama hicho,
aliipongeza kampuni ya Airtel kwa uamuzi wake wa kudhamini michuano hiyo ambayo
imeweza kuleta hamasa kubwa kwa wananchi wa Zanzibar.
Alisema kabla ya michuano hiyo Zanzibar ilikuwa nyuma katika soka la
wanawake lakini kupata udhamini huo ari imeongezeka zaidi na tayari wanawake
wengi wamehamasika kutaka kucheza mpira wa miguu.
Naye Meneja Mauzo wa Airtel Muhidin Mikidad alisema
kuwa kampuni yake itaendelea kusaidia michezo hiyo kadri ya hali itavyokuwa,
ambapo amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuwaunga mkono
Jijini Mbeya, timu ya wavulana ya Mbaspo
Academy imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ya kuibua
vipaji vya wachezaji chipukizi baada ya baada ya kuifunga Uyole Alliance 4-3 kwa
changamoto ya mikwaju ya penati.
Mchezo huo uliamuliwa kwa penati kufuatia timu hizo kutoka
sare ya kufungana 3-3 katika muda wa kawaida wa dakika 90.
Katika mchezo huo ulipigwa juzi katika dimba la
kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ulishuhudia vijana wa Uyole Alliance kutoka
nje kidogo ya jiji la Mbeya wakijipatia goli la kuongoza katika dakika ya
saba baada ya Daniel Shaban kufunga kwa penati baada mchezaji wa timu hiyo
kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.
Mbaspo walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha katika
dakika ya 20 kupitia kwa Albinus Haule kabla ya Claud Alex wa Uyole Alliance kuandika
bao la pili timu yake dakika ya 42.
Mabao mengine kwenye mchezo huo yalipatikana dakika 82
kwa upande wa Mbaspo mfungaji Shadraki Sape,wakati bao la Uyole Alliance
lilipatikana dakika ya 88 mfungaji ni Claud Casto.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.