Mbeya yaichapa Temeke bao 2-0 michuano ya Airtel Rising Stars
- Kinondoni yaipunguza kasi Arusha
Timu ya Temeke ya wavulana imeshindwa kutamba mbele ya Mbeya baada ya kumkubali kichapo cha 2-0 kwenye mashindano yanayoendelea ya Airtel Rising Stars fainali za taifa zinazochezwa kwenye uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.
Kwenye mechi ya kwanza ya michuano hiyo iliyochezwa leo, Jumatano 7 Septemba – timu ya wasichana ya Kinondoni iliifunga Arusha 4-0. Kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa jana Jumanne 6 Septemba, Arusha waliwafunga Lindi 2-0. Magoli ya Kinondoni yalifungwa na Anna Audela dakika ya 35 kwa njia ya penati. La pili likifungwa na Maimuna Abasi dakika 39, la tatu Aisha Juma dakika ya 41 na la nne likifungwa na Vaileth Tadeo dakika ya 60.
Kwenye mechi ya Mbeya na Temeke, timu ya Temeke ndio walianza na kasi baada ya kuwa wameshinda mchezo wa kwanza 4-1 dhidi ya Kinondoni, lakini mabeki wa Mbeya walisimama imara na kudhiti washambualiaji wa Temeke. Kwa dakika takribani 20 za kipindi cha kwanza, timu ya Temeke waliweza kuwadhiti vizuri Mbeya na hivyo kusababisha mpira kuchezwa nusu ya uwanja.
Hata hivyo, kadri muda ulivyokuwa unaenda, timu ya Mbeya iliweza kuanza mashambulizi taratibu na ilipofika dakika ya 45, Mbeya waliweza kuonana vizuri na kucheza pasi za uhakika ambapo Lameck Juma alitoa pasi nzuri kwa Ernest Kamange ambaye alimpiga beki wa Temeke na kuachia shuti lililomshindwa mlinda mlango wa Temeke na hivyo kuiandikia timu yake bao la kwanza. Timu zilienda mapumziko Mbeya ikiwa inaongeza 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Temeke wakitafuta bao la kuzawazisha. Hata hivyo kwenye dakika ya Ernest Kamange alifanyiwa madhambi kwenye nje kidogo na eneo la penati ambapo mwamuzi wa mchezo aliamuru ipingwe foul. Alikuwa na Lameck Juma ambaye alienda kucheza hiyo foul ambapo aliachia shuti lililoenda moja kwa moja hadi kimiani. Baada ya bao hilo, Temeke waliendeleza mashambulizi lakini yote yaliishia au kwa mabeki au kwa mlinda mlango ambaye alionyesha mpira wa kuvutiwa. Mpaka dakika ya 90 Temeke 0 Mbeya 2.
Fainali za Airtel Rising Stars 2016 zilifunguliwa jana Jumanne 6 Septemba na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Mkuu huyo wa Ilala alitoa Shukrani kwa kampuni ya Airtel Tanzania kuweza kuwekeza kwenye soka la vijana. ‘ Nataka nitoe pongezi za dhati kwa wenzetu wa Airtel kwa kudhamini mashindano haya. Hii inasaidia vijana kuweza kujipatia ajira kwani kwa wale watakaofanya vizuri watachanguliwa kujiunga na timu yetu ya vijana ya Serengeti Boys pamoja na Twiga stars, alisema Mjema. Aliongeza kuwa Wazazi wanatakiwa wawape watoto uhuru wa kuchangua fani zao na kusimamia bega kwa bega kuwaunga mkono.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema huu ni mwaka kwa Airtel kudhamini mashindano ya Airtel Rising Stars hapa nchini na kuhaidi kuendeleza udhamini huo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.