ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 1, 2016

LIVE KUPATWA KWA JUA NCHINI TANZANIA

11:33 Zaidi ya nusu ya jua imekwishafunikwa, kaubaridi kameanza. 

11:03 Takribani theluthi moja ya jua imefunikwa na  mwezi 9:48AM Watu waambiwa wajikusanye katika makundi yenye watu 30 ili wapewe vifaa vya kutazama kupatwa kwa jua 9:30am Mkuu wa wilaya Mbarali Rueben anawasili kwenye tukio na ulinzi usalama waimarishwa 9:21am  Umati wa watu wamiminika Rujewa, Mbarali kushuhudia kupatwa kwa jua kipete

11:03 Takribani theluthi moja ya jua imefunikwa  na mwezi

9:48AM Watu waambiwa wajikusanye katika makundi yenye watu 30 ili wapewe vifaa vya kutazama kupatwa kwa jua

9:30am Mkuu wa wilaya Mbarali Rueben anawasili kwenye tukio na ulinzi usalama waimarishwa

9:21am  Umati wa watu wamiminika Rujewa, Mbarali kushuhudia kupatwa kwa jua kipete

Viongozi wa serikali,  wanahabari wa ndani na nje ya nchi na wananchi wameshawasili katika eneo linalotumika kushuhudia kupatwa kwa jua.

Eneo hili lililopo Rujewa, Mbarali ambalo hutumika zaidi katika kuchimba mawe na kupasua kokoto leo limefurika watu ambao wapo hapo si kwa ajili ya kununua bidhaa hiyo ya ujenzi bali kusubiri kushuhudia tukio hilo la aina yake duniani.

Walimu wakiongozana na wanafunzi wa shule kutoka Mkoa wa Mbeya na jirani wamewasili hapa kama sehemu ya kuwafundisha wanafunzi kivitendo.

Askari wanarandaranda kila kona kuhakikisha usalama unaimarishwa.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala aliyewasili pia katika eneo hili, amesema tukio hilo limefungua fursa kwa kila mtu Mbeya hasa Mbarali.

Amevishukuru vyombo vya habari kwa kuutangaza mkoa  na amewaambia wananchi wajikusanye katika makundi ya watu 30 ili wapewe vifaa vya kutazama kupatwa kwa Jua Tanzania.

Makalla amewataka wananchi kuwa makini kuangalia tukio hilo akisisitiza "Huu siyo mwisho wa dunia."

Waendesha bodaboda na bajaji wanaendelea kuwaleta watu hapa Rujewa kushuhudia kupatwa kwa jua.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.