ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 14, 2016

KLINIKI YA MPIRA WA KIKAPU MWANZA YAFANA (YOUTH BASKETBALL CLINIC)

Mafunzo ya mpira wa kikapu kwa watoto na vijana (Youth baskeball clinic) yafanyika kwa siku mbili katika viwanja vya mpira wa kikapu kiloleli na uwanjawa CCM Kirumba. Mafunzo haya ambayo yaliandaliwa na Planet Social Development (PSD) pamoja na MRBA, yameendeshwa na Kocha George Ellis kutoka nchini Marekani kwa kushirikiana na kocha Bahati Mgunda kutoka kituo cha JMK Park cha Dar, Kocha Kizito Sosho Bahati wa kituo cha Kiloleli Mwanza na makocha wengine kutoka timu mbalimbali za hapa mkoani Mkoani Mwanza, pia makocha hawa wamesaidiwa na wachezaji mbalimbali ambao pia ni wachezaji wa timu ya Taifa na wengine wa Timu za hapa Mwanza. 

Wachezaji wa timu ya Taifa waliokuwepo ni Amon Diba Sembelya ambaye pia ni mchezaji wa Bugando Planet na Musheed Mudrikat.



Mafunzo haya ambayo yamefanyika kwa kushirikisha watoto  Zaidi ya 300 kwa siku mbili, ni sehemu ya mpango wa uendelezaji wa mpira wa kikapu wa miaka mitano kwa watoto na vijana kwa kanda ya ziwa wanaotoka katika shule za msingi na sekondari, ambapo kwa kuanza tumeanza kwa shule Jiji la Mwanza kwa maana ya Ilemela na Nyamagana.

Akizungumza wakati akiwa asawashiriki hawa, Kocha George amewataka washiriki wajifunze kila wakati na wasiogope kukosea kwani unapokosea ndio utakuwa na kitu cha kuendelea kukirekebisha, na pia amewataka kujifunza kutoka kwa mwingine kile ambacho mwenzako anakijua.

Vile vile kocha George amehaidi kuendelea kushirikiana na waandaji wa mafunzo haya ambapo kama ratiba itaenda sawa atarudi tena mwaka ni mwezi wa Aprili na kufanya mafunzo kama haya kwa siku nyingi tofauti na sasa,. Kwani amehamasika sana kwa kuona watoto wadogo wanajifunza mpira wa kikapu hasa katika uwanja wa Kiloleli.

Nae kocha bahati Mgunda ambaye anasimamia ligi ya NBA Junior katika kituo cha JMK Park amehaidi kuleta wachezaji kutoka katika kituo chake ili waweze kuja kushirikina kushindana na wenzao wa hapa mwanza na pia sasa tunafikiri kuwa na ligi ya watoto Tanzania nzima lakini kwa sasa tutaanza na mikoa ya Dar, Mwanza, Arusha na Dodoma.

Nao wachezajiwatimuyaTaifa Amon Diba na Mudrikat wame wataka watoto hawa kuwa na bidii ili waweze kuja kuwa wachezaji wakubwa.

Mratibu wa mafunzo haya, Kizito Sosho Bahati ambae pia aliwahi kuwa mchezaji wa timu yaTaifa mwaka 2005-2007, na pia alikuwa miongoni mwa makocha 20 watanzania walio kwenda nchini Marekani mwaka 2009 kwa mafunzo ya mchezo huu, amemshukuru kocha George kwa kufika Mwanza na kushirikiana na makocha wa Tanzania kuendesha mafunzo haya, lakini pia amepongeza mashirika/taasisi na watu mbalimbali waliojitokeza kusupor tufanyikaji wa Kliniki hii.

Namshukuru Mh. Angeline Mabula (MB) ambae Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi) kupitia taasisi anayoiongioza ya Angeline Foundation, halmashauri ya manispaa ya Ilemela kupitia kwa mkurugenzi wake John P. Wanga, SBC (T) Ltd (PEPSI), MOIL, shirika la Kijamii la MikonoYetu, kampuni ya BC ina baadhi ya wachezaji wa zamani ambao wameweza jikuchangia kufanikisha mafunzo haya.

Pia sasa tuna fiiri kufanya mafunzo kama haya kabla ya mwezi desemba ambapo tutakuwa pia na ligi ya shule za sekondari na ligi ya watoto wadogo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.