Na Annastazia Maginga, Mwanza.
ZANA mbalimbali za uvuvi haramu zenye thamani ya Sh milioni 106 zimetekezwa jana huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akiwatahadharisha wavuvi watakaobainika na nyavu hizo Mwezi Okitoba kuchukiliwa hatua za kisheria.
Zana hizo zimeteketezwa katika kata ya Nyakalilo iliyopo halmashauri ya Buchosa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza ambapo makokoro 53 yenye thamani ya Sh milioni 42.4, nyavu za timba 620 Sh milioni 43.4, kamba makokoro zenye urefu mita 33,000 zenye thamani Sh milioni16.5, nyavu za kuzamia 7 Sh laki 700,00 tupatupa 6 za Sh 120,000, kill net 20 sh laki100,000 pamoja na mitumbwi 15 sh milioni 3. Ilichomwa ili kuzuia uvuvi usiokuwa na tija kwa kuua mazalia ya samaki.
Akizungumza kwenye kampeni ya kupambana na uvuvi haramu Mongella aliwataka wavuvi hao kufuata sheria za uvuvi kwa kutumia zana zilizoruhisiwa na mamlaka husika ili kila mmoja aweze kunufaika na rasilimali zinazo patikana ndani ya Ziwa Victoria.
“Shughuli za uvuvi haramu zinaangamiza maisha ya viumbe hai wa majini na uchumi wa Mkoa kushuka kwa sababu Mkoa wetu unategemea shughuli za uvuvi ikiwemo wananchi wanaotegemea ziwa hili kufanya maendeleo”alisema Mongella.
Aidha aliwatahadharisha maafisa uvuvi na mali asili wa mkoa wa Mwanza kutojishusha na uvuvi haramu na kwamba atakayeshindwa kutekeleza agizo la kudhibiti uvui haramu atakuwa amejifukuza kazi mwenyewe.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kapole, alisema Sheria ya uvuvi namba22 ya 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 zinaelekeza nakuzuia matumizi ya zana haramu zauvuvi.
Halmashauri ya Buchosa ina jumlaya vituo 21 kwa ajiliya zoezi la ukusanyaji wa zana haramu ambapo vituo 20 vilivyobaki zana zenye thamani ya Sh milioni 229.7 zimekamatwa.
|
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.