ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 12, 2016

BASI LATEKETEA KWA MOTO SIMIYU - JEH SERIKALI NA HATMA YA HUDUMA YA ZIMAMOTO VIJIJINI.

Ajali ya kuungua moto kwa basi la Kampuni ya Katagi huko wilaya ya Itilima mkoani Simiyu imezidi kuwapa maswali mengi wananchi waishio vijijini na wilayani za maeneo ya mikoa mipya hapa nchini juu ya hatma ya mali na usalama wao pindi ajali ya moto inapojitokeza.

Basi hilo linalofanya safari zake toka kijiji cha Lagangabilili hadi mkoani mwanza kwa kiasi kikubwa limeteketea kwa moto jana majira ya mchana mara baada ya hitilafu za umeme kujitokeza ndani ya chombo hicho cha usafiri huku nyezo zilizotumika kuzima moto huo zikiwa ni zile za juhudi ya mkono kwa mkono toka kwa wananchi ambao walitumia mchanga, maji kwa njia ya ndoo kwani hakuna huduma ya zimamoto wilayani humo.


Bila jitihada za wananchi ambao walilishambulia kwa makundi zoezi hilo la uzimaji moto uliokuwa unaliteketeza basi hilo, hali ingekuwa tete zaidi kwa mali zisizo hamishika na miundombinu iliyokuwa pembezoni mwa basi hilo ambalo limeungua karibu na maduka kwenye moja ya kona kituo cha mabasi wilayani Itilima.







Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.