Na Annastazia Maginga,Kwimba.
ZAIDI ya watu 10 wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Super Shem kugongana uso kwa uso na daladala eneo la Nhungumalwa wilayani Kwimba mkoani hapa.
Ajali hiyo imetokea leo saa 12 Asubuhi wakati basi hilo lenye namba T- 874 CEW lililokuwa likitoka jijini Mbeya kuelekea jijini Mwanza kugongana na daladala namba T368 CWQ iliyokuwa ikitoka barabara ndogo ya Shilima ikielekea Nyegezi jijini Mwanza.
Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa ni dereva wa daladala aliyekuwa akitoka barabara ndogo ya Shilima akielekea Nyegezi kuingia barabara kuu bila kuzingatia sheria.
Akizungunza kwenye eneo la tukio mkuu wa wilaya ya Kwimba Mtemi Simion amesema kuwa majeruhi hao pamoja na marehemu walipelekwa hospitali ya wilaya Kwimba- Ngundu.
"Mara baada kutokea ajali majeruhi wote walikimbizwa hospitalini na watatu kati yao walipelekwa hospitali ya wilaya ya misungwi kutokana na hali zao kuwa mbaya lakini kwa bahati mbaya wawili kati ya hao walipoteza maisha wakati wakiwa njiani", alisema Simeon.
Kwa upande Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Kwimba-Ngundu Berthod Mchemba alikiri kupokea majeruhi 10 watano wanaume watano wa kike wakiwemo watoto wawili huku miili ya marehemu ikiwa 10.
"Kati ya majeruhi hao watatu wanahali mbaya na wamepelekwa hospitali ya rufaa bugando kwa ajili ya matibu zaidi ambapo wengi wao wana majeraha ya kuvunjika nyonga miguu pamoja na kutikisika kwa ubongo alisema", Mchemba.
Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo Eliza magambo amesema kuwa dereva wao hakuwa kwenye mwendo wa kasi labda kosa limetokea kwa dereva wa daladala (Hince) kuingia barabara kuu bila kuangalia kushoto na kulia.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka madereva kuwa makini kutokana na kupoteza nguvu ya taifa na kushusha uchimi wa nchi kutokana na kupoteza fedha nyingi kutibu majeruhi hao.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akiwataka madereva kuwa makini pindi wanapokuwa wanatumia vyombo vya moto.
"Mimi ni seme hii ajali ni ya kwanza tangu nihamishiwe mkoani hapa nikitokea Mbeya na imesababishwa na uzembe wa madereva haohao ambao kila kukicha tunakemea suala la uzembe huu," alisema Msangi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.