ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 25, 2016

WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU AWASILISHA MUSWADA WA KUTUNGA SHERIA YA WANATAALUMA WA KEMIA KWA KAMATI DODOMA

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (mbele aliye simama) akiongoza mkutano huo wa Kamati wakati wa kuwasilisha  muswada wa kutunga Sheria ya wanataaluma wa kemia mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika mkutano huo
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh.Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akifuatilia mkutano huo). Wengine ni maafisa wakuu wa ofisi ya Mkemia.
Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel V. Manyele (Katikati) akifuatilia mkutano huo wa Kamati mjini Dodoma
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Maendeleo ya Jamii, Mh. Peter Serukamba  (MB) akitoa miongozo kwenye mkutano huo wa Kamati mjini Dodoma
Baadhi ya wajumbe wa Kamati wakijadiliana jambo wakati wa mapunziko ya kamati hiyo ya Huduma za Maendeleo ya Jamii.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amewasilisha  muswada wa kutunga Sheria ya wanataaluma wa kemia mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii mapema jana tarehe 24 Agosti 2016 katika ukumbi wa mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali mjini Dodoma zinakoendelea  Kamati mbalimbali za Bunge.

Kamati hiyo ya Bunge ya kudumu ya Maendeleo ya Jamii inaongozwa na Mwenyekiti wake Mh. Peter Serukamba  (MB).pema

Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa kwenye mkutano wa nne wa Bunge utakaoanza tarehe 6 September 2016.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.