MWANZA.
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoa wa Mwanza umemtaka Mkurugenzi na wataalamu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuboresha miundombinu ya Soko Kuu la Kiloleli kama ilivyoagizwa na Rais Dk John Magufuli, hivi karibuni jijini Mwanza badala ya kuwahamisha kwa nguvu wafanyabiashara na kuwalazimisha kuhamia katika soko hilo ambalo miundombinu siyo rafiki kwao .
Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, Philipo Elieza alipotembelea katika Soko la Kiloleli na Soko la Kirumba kujionea miundombuni iliyopo kama inalizisha kuwezesha wafanyabiashara kuhamia pamoja na kuangalia endapo agizo la Rais Dk Magufuli tangu alitoe alipohutubia mamia ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara jijini Mwanza hivi karibuni.
Elieza aliwaleza wafanyabiashara aliowakuta katika soko la Kiloleli baada ya kulitembelea na ujumbe wake wa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa kutolidhishwa na hali ilivyo ambapo huduma ya vyoo haijaborshwa pamoja na maeneo ya wafanyabiashara wa mitumba kuwepo lakini hayajasakafiwa , kutokuwepo eneo zuri la wauza ndizi, nafaka na matunda ili kuwawezesha kuhamia.
“Haiwezekani soko hili la kiloleli likawa na huduma ya vyoo matundo manane kwa watu zaidi ya 500 watakaokuwa katika eneo hili wakifanya biashara zao lakini pia wamachinga maeneo yao hayajasakafiwa, wauza nafaka pia hawana majengo mazuri, wauza matunda hatujaona eneo likiwa limeboreshwa , wauza samaki wanalo eneo zuri, kwa ujmla bado muindombinu siyo rafiki kwa wafanyabiashara,”alisema.
Katibu huyo amemuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, John Wanga na wataalamu wake kutekeleza haraka agizo maelekezo ya Rais Dk Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella la kuboresha miundombinu ya soko hilo ili kuwa rafiki kuwezesha wafanyabirisha kuhamia kirahisi na kufanya shughuli zao katika mazingira yanayokubalika.
“Tumuombe Mkurugenzi Wanga atekeleze makubaliano ya awali kwa vitendo ya kulifanya soko hilo kuwa soko kuu la Kiloleli litakalouza matunda, ndizi, nafaka na mboga mboga kwa jumla badala ya masoko ya Kirumba na Sabasaba nayo kuuza kwa jumla na kushushiwa bidhaa hizo jambo ambalo limeonekana kupingwa na wafanyabiashara waliohamia soko la Kiloleli kwa kuwa si makubaliano sahihi,”alisema.
Elieza wamemuomba Mkurugenzi Wanga kumuwajibisha Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Ashimu Kimwaga kwa kushindwa kuwa mbunifu na mfatiliaji katika kuborsha miundombinu ya masoko hali inayowagawa wafanyabiashara na kuibua migogoro ya mara kwa mara na uchakavu wa huduma hafifu za shughuli za wafanyabiashara wadogo ikiwemo machinga badala ya kulitumia soko hilo siku ya Jumatano ya kila wiki ambayo hufanyika mnada (gulio).
Kwa upande wake Mkurugenzi Wanga amewataka wafanyabiashara kuwa watulivu katika kipndi hiki wakati Halmashauri ya Manispaa inaendelea na mchakato wa kumtafuta Mkandarasi wa kurekebisha na kuboresha miundombinu ya soko hilo ili kuwezesha kufanya shughuli zao kama walivyokubaliana na kuwataka wafanyabiashara wenye maeneo katika soko hilo kurejea.
"Tunasikitika kuona wafanyabiashara wenye wenye maeneo ambayo hayahitaji kuboreshwa nao wameyaterekeza na kukimbilia kufanya biashara katika maeneo mengine hivyo rai yangu kwao warudi katika maeneo yao tuliyowagawia ili kuepuka malalamiko yatakapo boreshwa tutayagawa kwa wale watakao kuwa tayari kufanya shughuli zao katika soko hilo,"alisisitiza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.