Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw.Said Meck Sadick ametoa agizo hilo mara baada ya kumtembelea mwanamke huyo ambaye amejifungua na kushindwa kumlea mtoto huyo ambaye mkuu huyo wa mkoa amelazimika kumchukua na kumpeleka kwenye kituo cha kulelea watoto cha upendo.
Amesema inasikitisha kuona mtuhumiwa huyo ambaye amemfanyia ukatili mwanamke huyo bado yupo mitaani huku akitishia familia na hiyo licha ya kukamatwa na kuachiwa kwa dhamana.
Baba mzazi wa msichana huyo Bw.Aloyce Lyimo analaani kitendo hicho na kusema kuwa kwa sasa hana uwezo wa kumtunza msichana huyo na mtoto wake baada ya kutumia gharama kubwa ikiwemo kuuza mali zake kwa ajili ya kumpatia matibabu.
Nao baadhi ya majirani wanaiomba serikali kumchukulia hatua mtuhumiwa huyo ambaye yuko mtaani kwa kuwa wananchi wa kijiji hicho wanaishi wa wasiwasi mkubwa.
Msichana huyo ambaye pia ana ugonjwa wa akili anamweleza mkuu wa mkoa kuwa hali yake kwa sasa inaanza kuimarika jambo kidondo hakijapona.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.