Katibu wa Chama cha Wakuilima wa Pamba Wilayani Kahama (TAKOGA) Paul Ntelya ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake nakudai kuwa wakulima hao wamekuwa wakitozwa asilimia tanoya mauzo ya Pamba yao kwenda Halmashauri ya Wilaya lakini wamekuwa hawatengenezi miundombinu.
Katibu huyo wa Takoga aliiomba pia Serikali kuhakikisha kuwa inavifufua viwanada vya Pamba vilivyokufa ilikuweza kumrahisishia Mkulima kulima Pamba yenye tija huku akiwa na na uhakika kupata masoko kwa urahisi hali ambayo inaweza kuchangia kuongeza uzalisha mara dufu kuliko ilivyokwa sasa.
Mmoja wa Walima wa zao hilo kutoka katika kata ya Idahina katika Halmasahauri ya Ushetu Juma Makashi aamesema kuwa licha ya msimu wa zao la Pamba kufunguliwa juni 21 lakini hakuna Makampuni yamegoma kununua Pamba hiyo kwa bei elekezi ya Serikali ya shilingi 1000 kwa kilo na badalayake Makampuni hayo yanataka kununua kwa bei ya shilingi 800.
Aidha Makashi amesema kuwa kutokana na hali hiyo wakulima wa Pamba wameamua kukaa na Pamba yao majumbani kwa kuwa bei hiyo haina tija kwao na hivyokupelekea kusimama kwa shughuli za kiuchumi hali ambayo pia imesababisha hata wanafunzi kusimama kwenda shule kutokana na wazazi waokutokuwa na fedha.
Pia ameongeza kuwa kuna tetesi za kuwa na Walanguzi wanaonunua Pamba kwa bei ya shilingi 700 kwa kuwabana Wakulima kutokana na kuwa na ugumu wa maisha hali ambayo wakulima hao tayari wameishaanza kuuza ilikukidhi mahitaji yao ya Msingi.
Nae Mkaguzi wa zao la Pamba Wilayani Kahama Emmanuel kilewo alipoulizwa kuhusu hali hiyo alisema kuwa tayari vikao vilikuwa vinaendelea baina ya Bodi ya Pamba pamoja na Wanunuzi nakuongeza kuwa makubaliano yanaenda vizuri na tayari baadhi ya Makampuni ya ununuzi yameanza kupeleka vifaa katika sehemu husika tayari kwa kuanza kazi hiyo.
Kilewo pia amesema kuwa kuhusu Walanguzi wa zao hilo katika masoko yaliopo Vijini, Serikali haiwatambui kama ni wanunuzi nawanakwenda kinyume cha Sheria na kuwataka Wakulimakutoa taarifa za kuwepo kwa watu hao ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.