ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 25, 2016

WAKALA WA KONYAGI KANDA YA ZIWA SASA KUJISHINDIA GARI KUPITIA SHINDANO LA 'NUNUA UZA SHINDA NA KONYAGI'

-Lori 2 kutolewa kwa washindi

Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji maarufu cha Konyagi na jamii zake,  JANA ilizindua kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji wa bidhaa zake Kanda ya Ziwa  itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu.


Kanda hiyo ya mauzo inajumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera, Geita, Simiyu Mbeya,Iringa,na  mikoa ya Kusini mwa Tanzania



Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Gold Crest jijini Mwanza, Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe  alisema “Dhumuni kuu la kampuni yetu ya TDL kuzindua kampeni ni  kuwainua wasambazaji wa biashara zetu. Katika kufanikisha suala hili wasambazaji wetu 2 watakaoibuka kila mmoja atajishindia lori jipya la usambazaji vinywaji aina ya Eicher lenye uzito wa tani 3”. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Matha Bangu - Brand Manager wa Konyagi akizungumza na wandishi wa habari jijini Mwanza (hawako pichani) 

Pia alisema kuwa wasambazaji wa bidhaa za kampuni wataweza kujishindia zawadi mbalimbali katika kipindi hiki cha kampeni lengo kubwa ni kuwawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi na kuongeza mapato yao ikiwemo kuchangia maendeleo ya kichumi nchini pamoja na jamii kwa ujumla.


 Bwana  Kavishe alisema katika shindano hili  wasambazaji wa bidhaa za TDL wamewekewa viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo kubwa ya kupata mshindi itakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa 10. “Tunaamini kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao wataongezea chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”.





Deogratius Magambo - Msambazaji wa Bidhaa za TBL wilaya ya Biharamulo na Ngara mkoani Kagera.
Msikilize mwakilishi huyu wa wasambazaji, anazungumzia nini kuhusu shindano na hatua za kampuni walizofanya kwa wafanyabiashara na wasambazaji. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe (wa pili kutoka kulia) akizungumza na wandishi wa habari, wengine kulia ni Matha Bangu Brand Manager wa Konyagi, Pascal Tesha Afisa biashara TDL (wa kwanza kushoto) na Deogratius Magambo - Msambazaji wa Bidhaa za TBL wilaya ya Biharamulo na Ngara mkoani Kagera.

Kusanyiko.

Wasambazaji toka maeneo mbalimbali Kanda ya Ziwa wamekusanyika hapa kwaajili ya kuwasilisha changamoto zao, sanjari na kupewa somo namna ya kuboresha shughuli zao.

Gari litakalo shindaniwa.

Mmoja wa mawakala akichangia ndani ya kusanyiko lililofanyika Gold Crest Mwanza.

Mawakala wakichangia ndani ya mkutano.

Maswali na majibu kibiashara zaidi.

Nunua, Uza, Shinda na Konyagi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.