Mshambuliaji nyota wa Chelsea, Diego Costa anadaiwa kutaka kuondoka Stamford Bridge na kujiunga na Atletico Madrid. Taarifa zinadai kuwa klabu hiyo ya Ligi Kuu inafahamu nia ya mshambuliaji huyo na tayari wameshakataa ofa ya kwanza iliyotolewa na Atletico. Meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte anatarajiwa kumshawishi Costa abakie katika klabu hiyo, kutokana na timu hiyo kushindwa kusajili mshambuliaji wa aina yake mpaka sasa. Costa amebakia kuwa chaguo la juu la Atletico na klabu hiyo ya Hispania inatarajiwa kutoa ofa nyingine kabla ya kufungwa kwa dirisha la majira ya kiangazi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.