Madereva hao wa njia ya Buhongwa-Pasiansi, Buhongwa-Airport na maeneo mengine ya Kishiri na Nyegezi jijini Mwanza waligoma leo majira ya saa 3 asubuhi hadi 7 mchana kupitia malalamiko yao ya kudai kunyanyaswa na askari polisi wa usalama barabarani kupitia faini wanazotozwa wakisema kuwa hazina vichwa wala miguu (ni za kubambikiziwa).
Sanjari na hayo lingine jipya madereva hao wameliibua wakisema kuwa hata malipo ya faini hizo wanazotozwa ni mradi wa wachache kwa kuwa risiti wanazopewa ni za miaka iliyopita na si zile za kielektoniki kama Serikali inavyoagiza.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Barabarani Robert Hussein akiwa ameambatana na mkuu wa upelelezi Agustin Senga ilibidi kufika eneo la tukio kujionea hali halisi ikiwa ni pamoja na kuzungumza na baadhi ya wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri, kuwasihi huduma zipate kurejea kama ilivyo ada wakati madai yao yakiendelea kufanyiwa kazi.
Kutokana na kutokubaliana na kupishana kauli baina na jeshi hilo na madereva wa daladala hali ilikuwa si shwari kwa kipindi kwani jeshi hilo lililazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya baadhi ya wapiga debe pamoja na madereva ambao walikuwa wakizozana kupata suluhu huku baadhi yao wakikamatwa kwaajili ya hatua nyingine zaidi.
Kitu.....
Moja kati ya tuhuma zinazodaiwa kuwaingiza madereva hao kwenye mtego wa kupigwa faini ni pamoja na kupaki maeneo yasiyoruhusiwa.
Kutokana na kutokubaliana na kupishana kauli baina na jeshi hilo na madereva wa daladala hali ilikuwa si shwari kwa kipindi kwani jeshi hilo lililazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya baadhi ya wapiga debe pamoja na madereva ambao walikuwa wakizozana kupata suluhu huku baadhi yao wakikamatwa kwaajili ya hatua nyingine zaidi.
Patashika ......
Huduma za usafiri zimesimama eneo la Nyegezi jijini Mwanza kwa saa kadha, nao abiria wakilazimika kutumia usafiri mbadala usio salama.
Miongoni mwa mambo ambayo madereva, makondakta na abiria wanakubaliana ni pamoja na kupitiwa upya vituo vya kupakia abiria na kuegesha magari kutokana na ongezeko la idadi ya watu hivi sasa. PICHA ZOTE NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.