Tawi la Benki ya CRDB Nyerere limetoa msaada wa madawati 60 yenye thamani ya Sh milioni 5 shule ya msingi Nyanza |
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha akizungumza kwenye hafla hilo. |
Maafisa wa benki ya CRDB wakijitambulisha |
Viongozi wakiwa wamekalia madawati kwa kujumuika na wanafunzi wa shule ya msingi Nyanza baada ya kukabidhiwa msaada na uongozi wa tawi la CRDB tawi la Nyerere la Jijini Mwanza |
|
"Tumekabidhi madawati 60 ili watoto wetu wasikae tena chini ya sakafu" |
BENKI ya CRDB tawi la Nyerere jijini Mwanza imekabidhi madawati 60 yenye thamani ya Sh milioni 5 kwa shule ya msingi ya Nyanza iliyopo Kata ya Mirongo Jiji la Mwanza ikiwa ni kuunga mkono agizo la Rais Dk John Magufuli (JPM), kukabiliana na chamgamoto ya upungufu wa madawati uliopo.
Meneja wa tawi hilo, Naomi Mwamfupe, katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo, alieleza kwamba Benki ya CRDB imejiwekea utamaduni wa kushiriki masuala mbalimbali ya kijamii na kutekeleza sera yake ya kutenga asilimia moja ya faida yake kila mwaka kuirudisha kwa jamii ikiwa ni kuchangia shughuli za maendeleo.
Mwamfupe alisema kwa uhitaji mkubwa Benki hiyo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika sekta za Elimu ikichangia vitabu, ujenzi wa matundu ya vyoo, vifaa vya shule na mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, Afya hukarabati wodi za wazazi na watoto na kutoa vifaa vya hospital na Mazingira imekuwa ikichangia vifaa vya kufanyia usafi katika maeneo mbalimbali mkoani Mwanza.
“Tunaamini kwamba elimu peke yake inaweza kulikwamua Taifa kutoka katika wimbi la umasikini kwa kupata maendeleo endelevu pale tu ambapo nchi itakuwa na miondombinu ya elimu iliyoimarika na kuwezesha wanafunzi wa shele za msingi, sekondari na vyuo vikuu kupa elimu bora,”alisema.
Meneja Mwamfupe ameiomba serikali ya awamu ya tano kuhamasisha pia ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kubanana madarasani kwa wingi pamoja kuwepo utekelezaji wa kuhakikisha wanakaa kwenye madawati ili kutoa fursa kwa walimu kufundisha na kuendana na kasi ya ongezeko la wanafunzi wengi kupata elimu nchini.
Naye mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhiwa madawati katika shule ya Nyanza, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, alipongeza uongozi wa tawi hilo na kutoa rai kwa wadau mbalimbali zikiwemo sekta binafsi wilayani humo kujitokeza kuunga mkono juhudi za serikali katika maendeleo na upatikanaji huduma bora za kijamii kama ilivyofanywa na CRDB.
“Wilaya katika kutekeleza agizo la Rais Dk Magufuli la kumaliza changamoto ya upungufu wa madawati tumeweza kutekeleza kwa asilimia 92 hadi sasa na kupitia msaada huo namba ya upungufu inazidi kupanda kutoka asilimia 8 iliyobaki hadi kufikia asilimia 7 ambapo shule hiyo imebaki na upungufu wa madawati 68 tu, rai uongozi wa shule mtaendelea kushirikiana na kamati za shule na wadau kukamilisha,”alisema Tesha.
Awali Mkuu wa shule ya Nyanza B, Juvenille Kaiza, kwa niaba ya wakuu wa shule za Nyanza A na C, walimu pamoja na Kamati za shule zilizowakirishwa na Mwenyekiti moja Badrudin Nsubuga alieleza changamoto mbili zinazoikabili shule hiyo kuwa ni pamoja na kujaa kwa shimo la maji taka na kusababisha huduma hiyo kutolewa kwa kuhofia magonjwa ya kuambukiza na kutokuwepo uzie eneo la mbele ya majengo ya utawala na madarasa ili kusaidia wanafunzi kutotoroka wakati wa masomo na ulizi wakati wa usiku.
Katika hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula (CCM), Diwani wa Kata ya Mirongo, Hamidu Seleman Said (CCM), mwenyekiti wa Kamati ya shule Nyanza B kwa niaba ya kamati ya shule A na C Badrudin Y. Nsubuga, mkuu wa shule ya Nyanza A Juvenille Kaiza, walimu na baadhi ya watumishi wa Benki ya CRDB Tawi la Nyerere.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.