ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 11, 2016

WAKURUGENZI MWANZA WAKALIA KUTI KAVU.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella .
Wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa wa Mwanza ambao hawajatimiza hata nusu ya idadi ya madawati yanayohitajika, wameagizwa kuhakikisha wanakamilisha  kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Akizungumza na madiwani wa Manispaa ya Ilemela juzi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema ameunda kamati kufuatilia utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la ifikapo mwisho wa mwezi huu wanafunzi wawe wanakaa kwenye madawati

“Anayependa kuendelea kushikilia nafasi yake ahakikishe halmashauri inafanya kazi usiku na mchana, ili kukamilisha idadi ya madawati,” alisema Mongella na kuongeza:

“Ole wake mkurugenzi ambaye tutakuta watoto wanakaa chini kwenye shule za halmashauri yake.”

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.