ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 14, 2016

SERIKALI BADO HAIJAKAMILISHA AHADI KWA WATU WENYE ALBINISM.

Mnara huu wa kwanza wa kihistoria dunia umesimikwa katika kipita shoto kikuu kinachounganisha barabara zinazoelekea mkoa wa Geita, Kahama, Bukoba mkoani Kagera na Kamanga mkoani Mwanza, ukiwa umeorodheshwa majina takribani 72 ya watu wenye albinism waliouawa.
Siku moja baada ya Maadhimisho ya Kimataifa ya Watu wenye ulemavu wa ngozi kuweza kufanyika katika maeneo mbalimbali huku kitaifa hapa nchini yakifanyika kwenye viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es salaam, miongoni mwa mikoa inayotajwa sana kuwa na kiwango kikubwa cha mauaji ya watu wenye albinism ni Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Hii leo Jembe Fm kupitia kipindi cha Kazi na Ngoma kinachoruka hewani kila siku saa 5 asubuhi hadi saa 7 mchana ilipata nafasi ya kuzungumza na Msemaji Mjumbe Mwakilishi Kitaifa Mkoa wa Shinyanga katika Chama cha watu wenye ulemevu nchini Bwana Kulwa Malenda.

MOJA YA MASWALI ALIYOULIZWA;-
-Maadhimisho kwa mkoa wa Mwanza yamekwendaje?
-Kesi kubwa iliyolindima mwishoni katika sakata la watu wenye albinism na kutikisa kila pande ni ile ya Mtoto Upendo, Juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kupambana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) Jeh Zinaridhisha?
-Vipi kauli yake  inafsi kuhusu maamuzi ya kesi na hukumu zitolewazo?  

BOFYA PLAY SIKILIZA MAHOJIANO ALIYOFANYA NA MANSOUR JUMANNE 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.