WANANCHI wa mji mdogo wa chalinze,Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani walikuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya usafiri pindi wanapoumwa wamepata mkombozi baada ya kupatiwa msaada wa gari jipya la kubebea wagonjwa na Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kwa lengo la kupunguza adha waliyokuwa wanaipata ya kutembea umbali mrefu.
Gari hilo la wagonjwa limekabidhiwa katika halfa fupi iliyofanyika katika kituo cha afya Chalinze,ambalo litaweza kuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo la chalinze kutokana na hapoa awali walikuwa wanapata usumbufu mkubwa pindi wanapoumwa kutokana na upatikanaji wa gari ulikuwa ni mgumu.
Akizungumza katika Makabidhiano hayo Ridhiwani alisema kwamba ameamua kutoa msaada wa gari hilo kutokana na kuona wananchi wake walikuwa wanapata shida kubwa ya usafiri pindi wanapokuwa wagonjwa hivyo gari hilo litaweza kutoa huduma kwa wakazi wa eneo hilo la chalinze na maeneo mengine ya jirani.
“Mimi kama mbunge wenu wa jimbo la chalinze nimegiswa sana katika suala hili kwani wananchi wangu walikuwa wanapata usumbufu mkubwa sana, hususani wakinamama wajawazito lakini kwa kuona umuhimu wake nimeweza kujitahidi na kuwaletea gari hili amablo nina imani litakuwa ni mkombozi kwani litawasaidia sana na mimi nitahakikisha ninaendelea kushirikiana na ninyi ili kuweza kuboresha huduma ya afya,”alisema Ridhiwani.
Aidha Ridhiwani alisema kwamba nia yake kubwa mbali na kutoa msaada huo wa gari la kubebea wagonjwa pia atahakikisha anaboresha sekta ya afua katika jimbo zima la chalinze katika zahanati na vituo vyote vya afya ili kuweza kuwapa fursa wananchi waweze kupata huduma ambayo inastahili pamoja na matibabu.
Pia alisema sambamba na hilo atahakikisha anapambana viivyo kuhakikisha kuna kuwepo na vifaa tiba katika maneneo husika pamoja na kuongeza idadai ya wauguzi kwani anatambua bado kunachangamoto nyingi katika sekta ya afaya hivyo atajitahidi kadiri ya uwezo wake ili kuongeza kasi ya kuboresha huduma hiyo ya afya.
Katika hatua nyinge Ridhiwani alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa kilio cha siku nyingi cha wananchi wa chalinze kutozwa gharama kubwa ya kuchangia usafiri pindi wanapoumwa kuanzia mwezi huu hakutakuwa na mchango wowote ule na gharama za usafiri pamoja na mafuta ofisi ya mbunge itagharamia yenyewe na sio wananchi tena.
Awali akisoma Risala katika hafla hiyo ya makabidhiano Mganga mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Rahim Mangai alisema kwamba kipindi cha nyuma wagonjwa walikuwa wanapata shida kubwa ya usafiri na wakati mwingine walikuwa wanajikuta wanashindwa kwenda kupatiwa matibabau kwa muda wa muafaka.
Pia alisema kwamba kituo hicho cha afya Chalinze bado kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mashine ya kufulia nguo za wagonjwa , uchakavu wa majengo ya wodi ya watoto,jengo a huduma ya mamam na mtoto, pamoja na ukosefu wa vifaa vya matibabu hususan kwa wagonjwa ambao ni wajawazito.
Nao baadhi ya wananchi wa eneo hilo la Chalinze akiwemo Amina Said pamoja na Maria Joseph walisema kwamba hapo mwanzoni walikuwa wanapata shida kubwa sana na wakati mwingine wanazeza kujifungulia nyumbani au njiani kutokana na tatizo la usafiri.
Aidha wamempongeza Mbunge wa Jimbo hili Ridhiwani Kikwete kwa kuweza kuwaondolea gharama za uchangiaji wa mafuta, kwani suala hilo kwa upande wao lilikuwa ni kero kubwa kwani wakati mwingine walikuwa wanaumwa lakini walikuwa washindwa kuchangia mafuta kutokana na kutokuwa na fedha yoyote.
“Kwa kweli sisi wananchi wa Chalinze tunampongeza Mbunge wetu na Mungu ambariki kwani hapao awali hususan sisi wakinamama tulikuwa tunajifungulia majumbani kweni na wengine hata njiani kutokana na shida ya upatikanaji wa usafiri lakini kwa sasa tumepatia gari hili la wagonjwa litaweza kutusaidia sana,”walisema wananchi hao.
WANANCHI wa mji mdogo wa chalinze kabla ya kupatiwa msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa walikuwa wanachangishwa fedha kwa ajili ya usafiri wa kuwapeleka kupatiwa matibabu zaidi katika hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa Tumbi, ambapo kuanzia Julai 1 mwaka huu watakuwa hawachangii gharama yoyote.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.