TBL,Mawnza yashinda Tuzo ya teknolojia ya kisasa Duniani.
Kiwanda cha bia cha TBL mwanza kimejishindi tuzo ya
teknolojia ya kisasa ya kuzalisha mvuke unaotumika katika upishi wa bia ,tuzo
hiyo imetolewa huko nchini London na kampuni ya ushindani na utafiti
ya SIB Miller kutoka nchini humo
viwanda vingi hushindanishwa ili kupata kiwanda ambacho kinao uwezo wa
kukidhi vigezo.
Tuzo hiyo ya Uvumbuzi
wa Teknolojia mpya iliandaliwa na Thomas
Bruwer ambaye ndiye alikuwa anaendesha
mradi wa DDH ( dry dehiscing) na kushirikisha viwanda takribani vyote Duniani.
Akizungumza na Vyombo vya habri jijini Mwanza
Mkurugenzi wa ufundi wa TBL Bwana
Gavin Van Wisk amesema
tuzo hiyo wameipokea siku chache kutoka nchini London, amewashukuru sana
wafanyakazi wote wa TBL Mwanza kwa
kuhakikisha wamejishindia tuzo hiyo na hiyo ni kutokana na juhudi zao kama
wafanyakazi.
Aidha Bwana Pitso amesema hivi sasa kwa uzalishaji wa bia katika
ushindani wa kidunia wamekuwa ndani ya washindi kumi bora wa kimataifa wa uzalishaji,wakati kwa Africa
wamekuwa wazalishaji wa bia yenye ubora yenye ubora kuliko kiwanda chochote.
Akizungumza na G sengo Blog Bwana Osca Kilasi ambaye ni meneja wa Ubishi kutoka Mwanza amesema
mradi umesaidia kupumguza matumizi ya dizeli , umeongeza uwezo wa kiwanda
kuzalisha,hata katika mazingira mradi huo unapunguza uharibifu wa
mazingira, lakini mzunguko wa wa wapishi umekuwa mfupi kutoka masaa mawili na dakika sabini hadi masaa mawili na dakika hamsini,hata katika eneo la gharama za umeme umepunguzo kwa kiasi kikubwa matumizi
ya Umeme,
“ Hii ni teknologia ambayo
itaenda viwanda vingine na teknolojia
hii unachukua shairi unatoa maganda na yale maganda yanatumika kwenye boiler kwa ajili ya
kuzalisha mvuke,hii inasadia bia kuwa nzuri,inakaa zaidi sokoni na inachujika
kirahisi baada ya kutumia mafuta
wanatumia maganda ,hii hufanya bia kukaa kwa muda mrefu sokoni” Alisema Oscar
Hata hivyo wakati akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya
Wafanyakazi bwana Pitso Gabriel (plant Manager) amesema Wao kama timu ya Mwanza wamefurahi hasa kwa
uzinduzi wa teknolojia na namna ilivyoleta matunda katika uzalishaji.
“ Zawadi hii itawafanya hata kuongeza nguvu ya uzalishaji na
hata hivyo ushindi huu umetuongezea ujasiri wa kufanya kazi kwa juhudi na
kujituma ili kuhakikisha hata mwakani tunaongeza tuzo nyingine nyingi” alisema
Pitso
Teknolojia hii ili kiwanda kiweze kutuitumia ni lazima
waombe kibali kutoka TBL Mwanza na taarifa zinasema kuwa baadhi ya viwanda
kutoka Nigeria na Nampula tayari
wameomba kutumia teknolojia hii ya kisasa na kipekee duniani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.