Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (Katikati) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,(hawapo pichani)wakati wa kutangaza ujio wa Mwanamuziki nguli kutoka nchini Marekani NE-YO, atakayewasili nchini Mei 19 na Mei 21 atatoa burudani katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka Festival 2016 liloandaliwa na kampuni ya Jembe chini ya udhamini mkuu wa Vodacom Tanzania, kushoto ni Msimamizi Mkuu wa Itifaki wa Jembe Media Limited, Leah Guya na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa Tamasha hilo, Costantine Magavilla. |
Ni wakati mwingine tena Vodacom Tanzania inawaletea burudani wateja wake na watanzania wote kwa ujumla, Ili waweze kufurahia kwa pamoja kwa kufanikisha hili sasa Vodacom Tanzania, Kushirikiana na Jembe Media Limited tumeamua kumleta mwanamuziki nguli kutoka nchini Marekani NE-YO ambaye ataingia hapa nchini mnamo mwezi huu tarehe 19.
NE-YO atawasili nchini kwa ajili ya kutoa burudani ya aina yake katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka na Vodacom 2016 chini ya udhamini mkuu wa Vodacom Tanzania.
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema Vodacom wameamua kumleta mwanamuziki huyu wakiwa na zaidi ya sababu kuu tatu alisema Nkurlu.
1. Kwa ajili ya kuwapatia burudani ya kimataifa wateja watu na watanzania wote kwa ujumla kupitia tamasha la Jembeka 2016.
2. Kuwaunganisha wasanii wetu nchini na msanii huyo wa kimataifa ili waweze kufanya kazi siku za usono nasi tuweze kuutangaza muziki wetu katika Nyanja za kimataifa.
3. Kushiriki katika shughuli za kusaidia jamii kupitia taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation hapa nchini.
4. Kutambulisha shughuli mbalimbali za uchumi hasa Utalii wa mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla kupitia kampeni ya 'I Love Rock City' inayoendeshwa sanjari na burudani ya uelimishaji katika mitaa mbalimbali ya mkoa huo, vitongoji na wilaya zake kuelekea tamasha hilo kubwa la Burudani (JEMBEKA FESTIVAL 2016)
Licha ya mkali anaye peperusha bendera ya Tanzania nje ya mipaka yake Diamond Platnumz kula shavu la kuwako stejini siku hiyo, pia jina la Kibra Sir Juma Nature lilihusishwa mapema kabisa katika mipango ya tamasha hilo kutokana na maombi ya mashabiki wa jiji hilo la Miamba na vitongoji vyake kupitia ujumbe mfupi/ sms za vipindi tofauti tofauti ndani ya Jembe Fm kiasi cha kuipa presha kamati husika kumuweka mkali huyo kwenye listi ya wakali watakaopanda jukwaa moja na Neyo.
Wapo wakali wengine wanaotamba watakaozuka tamashani na kumwaga burudani ambao ni pamoja na mzawa wa Mwanza 'Ngosha The Don' aka Fid Q, Mr. Blue, Nay wa Mitego, Baraka Da Prince, Stamina, Mo Music, Ruby, Maua Sama, Skylight Band na JJ Band.
Wengine kutoka Rock City ni Biznea, Jimmy Chansa, Cooly Chata, Future JNL, Mc Coyo, Young Rafa, Dogo Dee, King Silver na wengine kibao.
Aidha ma Dj toka himaya ya burudani ndani ya 93.7 Jembe Fm Mwanza wanaojulikana kama 'Jembe Djz' ndiyo ambao wamepewa dhamana ya kuhakikisha kiu ya muziki safi wa kiushindani unahusika siku hiyo ndani ya eneo la tukio Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kiingilio cha Shilingi 10,000 Silver, 50,000 Gold na 100,000 kwa Platnum.
JEMBEKA FESTIVAL 2016 Imedhaminiwa na Vodacom Tanzania! Vodacom Kazi ni Kwako. Special Thanks FastJet, EF Outdoor, Ndege Insurance, Syscorp Corporation, KK Security, Jembe Fm, JembeniJembe, Gsengo Blog, Michuzi Blog, Binagi Blog na wadau wengine.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.