ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 4, 2016

HANS POPPE ASHANGAZWA NA JERRY MURO KUCHANGANYIKIWA BAADA YA YEYE KUELEZA RUSHWA LIGI KUU

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema ameshangazwa na Msemaji wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro kujishitukia baada ya yeye kusema mwishoni mwa ligi, kuna michezo ya rushwa na akaitaja aina yake.

Hans Poppe amesema ameona Muro akihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari na kusema anataka kumpeleka Takukuru ili akaeleze kuhusiana na rushwa.

“Lakini kinachonishangaza ni kitu kimoja, mimi sikutaja jina la mtu wala timu. Utaona nilifanya mahojiano na gazeti la Championi, hata ilivyoandikwa sikutaja klabu wala jina la mtu, sasa unapomsikia mtu wa sehemu fulani anakurupuka na kusema kitu, huoni hii ni hofu.

“Nimeshangazwa sana kusikia mtu anahojiwa, anajitaja, analalamika wakati hakuwa ametajwa mtu,” alisema Hans Poppe.

“Hii inanikumbusha mwaka 1978, Uganda walikuwa wanarusha ndege zao za kivita zinaingia hadi anga ya Tanzania. Rais Nyerere akasema kuna watu ambao ni majirani zetu wanarusha ndege zao zinaingia ndani ya enero letu, nafikiri wanatutafuta.

“Siku iliyofuata Iddi Amini aliyekuwa Rais wa Uganda wakati huo akasema, sio mimi. Sasa ndiyo anachofanya huyu kijana hapa,” alisema.


Hans Poppe alihojiwa na gazeti la michezo la Championi na kueleza kuhusiana na suala la rushwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.