WANAMUZIKI NA WADAU WA MUZIKI KUKUTANA NA MKUU WA MKOA DSM
ALHAMISI HII
Wanamuziki wa dansi, taarab, bongo fleva na wadau wa muziki
waishio Dar es Salaam, Alhamisi hii watakutana na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
Mheshimiwa Paul Makonda ili kubadilisha mawazo juu mwenendo wa kazi zao.
Wasanii na wadau hao watakutana na Makonda ndani ya ukumbi
wa Vijana Social Hall Kinondoni kuanzia saa 5asubuhikatika mkutano
utakaohudhuriwa pia na wamiliki wa kumbi za starehe wa mkoa wa Dar es Salaam.
Mkutano huo umeandaliwa na kamati ya ushirikiano ya
wanamuziki wa dansi, taarab na wamiliki wa kumbi za starehe iliyoundwa hivi
karibuni ili kujadili kwa undani changamoto za sheria ya biashara ya vileo na
burudani ambazo ziko tangu mwaka 1968 na 1972.
Mmoja wa wasemaji wa umoja huo wa wanamuziki wa dansi,
taarab na wamiliki wa kumbi za starehe, Juma Mbizo, ameuambia mtandao huu kuwa
maombi yao ya kumwalika Mkuu wa Mkoa katika mkutano huo, yameshawasilishwa kwa
Mkuu huyo wa Mkoa.
Jumba Mbizo amewataka wanamuziki, wadau wa muziki na wamiliki wa
kumbi za starehe watakaopata taarifa za mkutano huo kwa njia yoyote ile, wafike
kwa wingi Vijana Social.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.