ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 22, 2016

GARI LANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO MCHANA HUU.

 Gari ndogo aina ya Nissan Xtrail  limenusurika kuteketea kwa moto mchana huu katika barabara ya Mwanza - Shinyanga eneo la Maliasili njia kuelekea Nyegezi. 

Mashuhuda wanasema kuwa hitilafu ya umeme ilitokea upande wa injini kwenye betri na motoukazuka. 
 Baada ya kutokea moto huo baadhi ya vijana waishio maeneo ya Igogo na karibu na eneo hilo walikimbilia gari hilo wakijidai kusaidia kuzima moto kwa kutumia mchanga na matawi huku wakingoa baadhi ya spea za gari hilo lililopata ajali.

Milipuko ya baadhi ya parts zilizokuwa zikiungua zilisababisha vijana hao kusambaratika. 
Licha ya Zimamoto kuchelewa kufika eneo la tukio lakini walifanikiwa kuuzima moto huo. PICHA NA ZEPHANIA MANDIA  WA GSENGO BLOG.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.