NA VICTOR MASANGU, RUFIJI
WANANCHI wa Wilaya mpya ya Kibiti Mkoani Pwani kwa sasa wanakabiliwa na tatizo kubwa la upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme, kwa kipindi cha muda mrefu jambo ambalo linakwamisha kwa kiasi kikubwa katika kuendesha shughuli zao za kimaendeleo.
Wakizungumza na kwa nyakati tofauti katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Ungando kwa ajili ya kuweza kutoa shukrani kwa kuchaguliwa kushika anafasi hiyo pamoja na kuweza kubaini changamoto mbali bali zinazowakabili wananchi wake ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Wananchi hao akiwemo Nuruel Moshi pamoja na Mohamed Ngogota walisema kwamba licha ya Kibiti kupandishwa adhi ya kuwa Wilaya lakini hali ya kiuchumi inazidi kuwa mbaya kutokana na watu wengine katika eneo hilo wanaendesha maisha yao kwa kutegemea nishati ya umeme hivyo.
Waliongeza kuwa kwa kipindi hiki wamejikuta wanashindwa kutimiza malengo waliyojiwekea kwani bidhaa zao nyingi kwa sasa zimeharibika ikiwemo samaki nyama, na maziwa, juice pamoja na mambo mengine kutokana na kukosa nishati hiyo ya umeme hivyo wameiomba serikali kulitafutia ufumbizi wa haraka suaa hilo .
Nao wakinamama ambao wanajishughulisha na biashara za kuuza chakula mbali mbali akiwemo Zawadi Mtunguja ambaye yeye ni muuguzi katika kituo cha afya Kibiti pamoja Judidhi Mlungu walisema kwa kutokuwepi kwa umeme kwa upande wao kumewaathiri kwa kisi kikubwa kwani biashara zao nyingine hazifanyiki hvyo wanapata hasara.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Ungando amewahakikishia wananchi wake kulishughulikia kwa hali na mali suala hio la umeme na tayari ameshalipeleka kwa uongozi wa mamlaka husisika na watalifanyika kazi na kuwataka wavute subira.
“Wananchi wangu natambua kuwepo kwa chanagmoto hii ya umeme na inawaumiza sana lakini kwa upande wangu nitajitahidi kuisimamia hili suala ili umeme uweze kuwa wa akika kwani natambau wananchi wa jimbo langu la kibiti wanafanya shughuli zao mbali mbai kwa kutegemea nishati hii ya umeme hivyo nitaifanyika kazi kwani nimeshalifikisha kwa viongozi wananaohusika,”alisema Ungando.
Aidha Mbunge huyo alibainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuweka mikakati kabambe ya kuwasaidia wananchi wake katika kujishughulisha katika shughuli mbali mbali za kuleta maendeleo hivyo kuwaomba madiwani na viongozi kushirikiana bega kwa bega ili kuweza kuleta mabadiliko chanya katika jimbo hilo.
HIVI karibuni Rais wa awamu ya tano Dr. John Pombe Magufuli alitangaza kuipandisha adhi Wilaya hiyo mpya ya Kibiti ambayo hata hivyo bado inaonekana kukabiliwa na changamoto nyingi katika sekta mbali mbali hivyo kupelekea wananchi wake kulalamika kutokana na kushindwa kupata huduma zinazostahili kwa wakati.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.