ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 14, 2016

TASWIRA ZA MAHAKAMANI KESI YA WENJE DHIDI YA MBUNGE WA SASA JIMBO LA NYAMAGANA NA EZEKIAH WENJE KATIKA MWANZA

Kutoka Mahakama kuu Kanda ya Mwanza leo hii ile kesi ya Uchaguzi iliyofunguliwa na Mbunge wa zamani Ezekiel  Wenje (CHADEMA) katika Jimbo la Nyamagana dhidi ya Mbunge wa sasa Stanslaus Mabula (CCM) kwenye kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015, kesi hiyo ililazimika kusimama katika awamu ya kwanza majira ya saa 6 mchana kisha ikaendelea tena mnamo saa 8 kwa kusikiliza mashahidi wa upande wa mlalamikaji.
Mbunge wa sasa Stanslaus Mabula (mbele kabisa kushoto).
 HALI ILIVYOKUWA.
Upande wa Mashahidi walianza kwa kutoa ushahidi na kiapo kilicho letwa na Wakili wa Mlalamikaji kilionekana kimejikita zaidi katikamaoni na si fact, maeneo hayo ni:- *Wenje kutaka kurejeshewa gharama za Uchaguzi.
*Matumizi ya Printing ambayo msimamizi wa Uchaguzi alikataa yasitumike.
*Hata hivyo jaji anayesimamia kesi hiyo amesema kuwa hata kama viapo hivyo vitaonekana vina mapungufu vitaondolewa na kesi itaendelea kusikilizwa kama kawaida.
Kesi itaendelea kusikilizwa kama kawaida tarehe 16/03/2016
Nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza wakati.

Katika hali nyingine polisi walilazimika kutumia virungu kuwatawanya wanachama wa CHADEMA waliofurika kwa wingi mahakamani hapo kushuhudia kesi hiyo tangu  asubuhi.
Polisi wakiwatawanya wananchi waliokuwa nje ya mahakama wakiimba na kuonyesha ishara ya vidole viwili kama inavyotumiwa na CHADEMA.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe akipewa utaratibu na mmoja wa askari wa jeshi la polisi Mwanza juu ya utaratibu wa kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
Maelekezo zaidi.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa huu ni msafara wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe (aliyevaa koti jeusi, shati jeupe na jeans) akiwa na mlalamikaji Ezekiel Wenje (suruali nyeusi na shati rangi ya maziwa) wakitoka mahakamani baada ya kesi hiyo kuahirishwa.
Wakitoka Mahakamani baada ya kesi kuahirishwa Mbunge wa sasa Stanslaus Mabula (kushoto) akiwa na Wakili wake Mhe. Mtalemwa.
Ni pilika pilika mtaani kila mmoja na hisia zake.
Mhe. Mbowe akiwa na wadau wengine wa CHADEMA juu ghorofani na chini ni wananchi waliowasindikiza hadi eneo hilo.
PICHA ZOTE NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG
ITAENDELEA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.