Msanii wa Kenya mwenye vipaji vingi, KING KANJA ameachia wimbo mpya CATHY akimshirikisha Ava Lov na Big T. Wimbo huu unakuja baada ya kuonesha uwezo wake kwenye tamasha la 2016 SXSX (South by South West) huko Austin, Texas.
Wimbo huu unaovutia na wenye vionjo vitamu ni mahsusi kwa wasichana kuwakumbusha kutafuta mafanikio na kujituma.
CATHY umetayarishwa na mtayarishaji wa hip hop na R&B aliyewahi kutajwa kuwania tuzo za Grammy, Chucky Thompson, ambaye pia alitayarisha One Mic ya Nas, na zingine zilizofanya vizuri.
King Kanja anasema, “Naipenda CATHY kwa sababu ya ujumbe wake. Kwa Waafrika wenzangu na Waafrika Mashariki wenzangu, nataka mfahamu najituma sana kwa Afrika na hasa nyumbani Kenya, 254” na kuongeza, “Wimbo huu ulihamasishwa na Cathy Hughes, mwanzilishi wa Radio One, niliyekutana naye na kufanya kazi kupitia mshauri wake, marehemu Tony Washington.”
Video ya CATHY imetayarishwa na 1ST Impressions na ilifanyika Miami, Florida. CATHY inaonesha ukuaji wa kimuziki na binafsi kwa King Kanja na kufanya kazi na Chucky kumeongeza ukuaji huo kama msanii.
Producer mahiri Drummaboy anasema, "Kaka, una kitu special mikononi mwako. "
Chuck "Jigsaw" Creekmur CEO & mwanzilishi wa All hip-hop anasema, "Nilijua niliposikiliza muziki kuwa ni wewe.”
Itazame CATHY kwenye Vevo: http://bit.ly/1nZjODi
Ipakue CATHY kwenye iTunes: https://itun.es/us/x4labb
Ipakue CATHY kwenye Mdundo: http://mdundo.com/a/18480
Tafadhali pata wimbo na artwork yake vilivyoambatatishwa kwenye email hii. Kuwa huru kusambaza kwenye mitandao yako.
DOKEZO KWA WAHARIRI:
KING KANJA anajulikana kwa kuweka pamoja hip-hop, R&B, reggae na muziki wa Kiafrika huku akiuchanganya pia lugha zake za nyumbani za Kikuyu na Kiswahili kwenye mashairi yake. Nyimbo zenye utambulisho huu zimemkusanyia mashabiki si tu Afrika, bali Ulaya, Asia na Marekani.
Akizaliwa London kwenye familia ya Wakenya na kukulia kwenye maeneo ya DMV (DC/Maryland/Virginia), alikotengeneza mtindo wake, KING KANJAamekuwa akifanya ziara duniani tangu akiwa na miaka 15 akisambaza nyimbo zake za kipekee.
King Kanja alishinda shindano la Wild Out Wednesdays la kwenye kipindi maarufu cha BET, 106 & Park. Mwaka 2015, KING KANJA alitumbuiza pamoja na msanii/mtayarishaji/DJ/engineer wa Uingereza, Silvastone kwenye tamasha la Legendary Glastonbury huko London.
Alishiriki kwenye Cypher ya msimu wa tatu wa Coke Studio Africa iliyofanyika Nairobi, Kenya. Cypher hiyo ilirushwa kwenye awamu ya mwisho ya kipindi hicho, iliyomshirikisha pia msanii wa Marekani na mshindi wa tuzo za Grammy, NE-YO. Alialikwa pia kutumbuiza kwenye tamasha la SXSW kwa mara ya kwanza mwaka 2015, huku akitarajiwa kurudi tena mwaka 2016 kama msanii maalum.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.