Mchezaji wa kimataifa, raia wa
Senegal, Demba Ba ni mchezaji nyota aliyewahi kukipiga katika vilabu vya
Newcastle, Chelsea na Besiktas kabla ya kuhamia timu ya sasa ya Shangai Shenhua
iliyomo katika ligi kuu ya China.
Mchezaji raia wa Zambia, Jacob
Mulenga (pichani) naye anacheza soka la kulipwa katika ligi kuu ya china katika
kilabu cha Shijiazhuang Ever Bright.
Gervinho baada ya kuchezea timu
za Arsenal ya ligi kuu ya Uingereza na AS Roma ya Italia alitimkia ligi kuu
nchini China ambako sasa anachezea ligi kilabu cha Hebei China Fortune. (PICHA
ZOTE KWA HISANI YA MTANDAO)
Kampuni ya StarTimes Tanzania imewaletea watanzania uhondo wa miongoni mwa ligi ambazo zinajizolea umaarufu kwa kasi hivi sasa duniani, ligi kuu ya China, kwenye chaneli zake za michezo na kuwafanya kufurahia kuona wachezaji nyota kutoka nchi mbalimbali.
Akizungumza juu ya habari hiyo njema kwa wapenzi wa soka nchini, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Lanfang Liao, amesema kuwa ligi hiyo imejizolea umaarufu mkubwa kutokana na wachezaji nyota waliowahi kucheza kwenye vilabu mbalimbali barani Ulaya kukimbilia huko.
“Tunayo furaha kubwa kuwafahamisha wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa tumepata haki miliki ya kuonyesha ligi kuu ya China kwa muda wa miaka mitatu mfululizo na kuonyesha jumla ya michezo takribani 240 moja kwa moja kutoka kwa timu 16 zinazoshiriki. Na tofauti na ligi zingine duniani, ligi hii yenyewe huwa inaanza kwenye miezi ya Machi (msimu wa vuli) na kumalizika Disemba (mapema msimu wa baridi).” Alisema Bw. Liao
Ligi kuu ya China inachukuliwa kuwa ni ya pili, baada ya ligi kuu ya Uingereza ikiitangulia ya Italia, Serie A kwa kuvutia wachezaji wa nje. Ligi hii inalenga kukuza ushindani wenye hali ya juu na pia kukuza ubora wa makocha na wachezaji wa kigeni ambao hatimaye wataweza kujiimarisha katika mfumo wa Uingereza na kuweza kusajili na kuuza wachezaji.
Bw. Liao aliongezea kuwa, “Tunafahamu kuwa watanzania wanapenda sana soka na kama waafrika kwa ujumla wanafurahia sana kuona wenzao wakiliwakilisha bara hili kimataifa. Ligi kuu ya China imejaa waafrika lukuki ambao wanatoka nchi jirani na zinginezo Afrika kama vile James Chamanga na Jacob Mulenga (Zambia), Assani Lukimya (DRC Kongo), Asamoah Gyan (Ghana), Gervinho (Ivory Coast), Demba Ba (Senegal) na nyota wengine kutoka nchi zingine waliowahi kucheza vilabu vikubwa kama vile Ramires, Jackson Martinez, Ezequiel Lavezzi, Paulinho na wengineo.”
“Natumaini kuwa kuja kwa ligi hii kutaongezea burudani ya kutoksha miongoni mwa wateja kwani tulivyokwishawaeleza wateja wetu kuwa siku zote tunapambana kuwapatia mambo mazuri zaidi. Tunafahamu wateja wanahitaji zaidi na zaidi na hata tukilinganisha na jinsi tulivyoanza na tulipofikia ni dhahiri kuwa tumefanya juhudi za kutosha katika kuboresha maudhui ya vipi vyetu. Mpaka sasa ligi ya Bundesliga, Serie A, Ligue 1 zote zinaonekana moja kwa moja.” Alihitimisha Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini
Naye kwa upande wake Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. David Kisaka aliongezea kuwa ujio wa ligi kuu ya China kwenye dikoda za StarTimes umekuja wakati sahihi kwani hivi sasa kuna punguzo kubwa la bei pamoja na ofa ya kuangalia vifurushi vya kawaida na michezo buro ikiwa ni shamrashamra za kuikaribisha sikukuu ya Pasaka.
“Katika kipindi hiki cha Pasaka tumeshusha bei za dikoda zetu za antenna kutoka 34,000/- mpaka 22,000/- tu na kwa upande wa dishi kutoka shilingi 88,000/- mpaka 86,000/- tu. Mteja akinunua bidhaa hizo atafurahia kifurushi cha bure cha chaneli za kawaida pamoja na cha Sport Plus ambacho ataweza kujionea mechi mbalimbali moja kwa moja pamoja na ligi hii ya China ambayo tumewafahamisha.” Alimalizia Bw. Kisaka

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.