ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 22, 2016

MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM APATIKANA.


Uchaguzi Meya Dar es salaam hatimaye umekuja na matokeo ambapo diwani Isaya Mwita wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo nchini (CHADEMA) ameibuka mshindi wa nafasi hiyo baada ya kuzitwaa kura 84 dhidi ya kura 67 za Yenga Omary-wa Chama Cha mapinduzi (CCM).

Kura 7 za uchaguzi huo zimeharibika.

NI - Wajumbe 163 walitarajiwa kushiriki zoezi hilo, 87 wakiwa ni kutoka muungano wa upinzani wa Ukawa na 76 kutoka chama tawala cha CCM.
Siku moja kabla yaani Jumatatu, Rais Magufuli alizitaka pande zote kukamilisha mchakato wa kumpata meya badala ya kuendelea kulumbana.
Dkt Magufuli alisema upande wowote unafaa uwe tayari kupokea matokeo ya uchaguzi huo, ili meya apatikane na jiji liweze kuendelea na mipango yake ya kuwahudumia wananchi bila vikwazo.

"Mahali tunapostahili kushinda kama tumeshinda tushinde kweli, lakini mahali tunaposhindwa napo tukubali kushindwa, na hiyo ndio demokrasia ya kweli" alisema Dkt Magufuli.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.