Keki ya uzinduzi wa duka jipya la Airtel lililopo ndani ya Rockcity shopping Mall jijini Mwanza. |
Airtel yazindua duka jipya ndani ya Mwanza Mall
· Wateja kufurahia huduma na bidhaa mbalimbali ikiwemo huduma ya Airtel Money
Mwanza, Tanzania Jumanne 15 Machi 2016, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua duka jipya la kisasa jijini Mwanza ndani ya Mwanza Rock City shopping Mall litakalowawezesha wateja wake kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Airtel wakati wowote wakiwa wanafanya manunuzi mbalimbali katika Mall hiyo
Duka hilo la jipya la Airtel Rock City Shop ni duka la tatu kuzinduliwa kwa mwaka huu kwa lengo la kuendelea kukamilisha dhamira ya Airtel ya kuongeza vituo vya kutoa huduma bora kwa wateja wake wanaoongezeka kila siku nchi nzima.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa duka hilo , Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Bi Adrian Lyamba alisema” Duka hili tunalozindua leo litaweza kuwahudumia wateja kutoka katika maeneo mbalimbali ya kanda ya ziwa watakaokuja kutembelea Rock City Mall kwa mahitaji mengine. kupitia duka hili pia tunawahakikishia wateja wetu usalama wa pesa zao kwani hawatakuwa na haja ya kubeba burungutu la pesa pindi watakapotembelea Rock City Mall kwa kuwa kupitia huduma ya Airtel Money wataweza kuweka au kutoa pesa pamoja na kufanya malipo mbalimbali wakati wote. Wafanyabiashara pia wanaweza kuweka pesa za mauzo yao ya kila siku kwa njia rahisi na salama kupitia duka letu hili jipya”
Lyamba aliongeza kwa kusema, duka hilo jipya litatoa huduma mbalimbali zikiwemo kuunganishwa na huduma ya intaneti, huduma ya Airtel Money, kurudisha namba iliyopotea, kufanya malipo ya ankra, kusajiri namba za simu, muda wa maongezi, kujipatia modemu zenye ofa kabambe, pamoja na simu za kisasa kabisa ikiwemo simu za Bravo Z10 inayokuja na ofa maalumu ya kifurushi cha intaneti kwa shilingi 75,000
Tunaamini duka hili litawawezesha wateja wetu kupata huduma zetu kwa urahisi sana wakati wowote wanapotembelea Mall. Aliongeza Lyamba
Akiongea wakati wa uzinduzi , Kamanda wa polisi Wilaya ya Ilemela, Switbert Kisha alisema “ napeda kuchukua fulsa hii kuwashukuru Airtel kwa kuongeza maduka yake na kuhakikisha wanawafika wateja wake kwa urahisi ili kutoa huduma bora za mawasiliano katika mkoa wa Mwanza.
Duka hili ndani ya Mall hii litawahakikishia watanzania usalama zaidi katika kutumia huduma ya Airtel Money hivyo nawapongeza sana Airtel kwa kuwahakikishia watanzanai usalama kupitia duka hili.
Huduma za mawasiliano ni chachu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi ya jamii na nchi kwa ujumla. Serikali inapongeza sana jitihada za Airtel nakuwaomba waendelee kutanua huduma za zaidi na kuwafikiwa watanzania wanaokaa maeneo ya pembezoni mwa nchi aliongeza.
Duka la Airtel ndani ya Rock City Mall Mwanza litakuwa likifunguliwa kuanzia saa 8 asubuhi mpaka saa 11 jioni siku za Jumatatu hadi Ijumaa na siku ya Jumamosi duka litafunguliwa kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 7 mchana
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.