AIRTEL FURSA YAFIKIA VIJANA WILAYANI NGARA
Mwanzoni mwa wiki hii Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa iliweza kufika katika kijiji cha Kumnazi wilayani Ngara mkoani Kagera na kumfikia Kijana Kanizio Annatory anayejishughulisha na biashara ya kuosha magari, kwa kumpatia vifaa na kufanyiwa ukarabati wa eneo lake la kazi . Vijana wengi wanaamini maisha mazuri na fursa za kiuchumi zinapatikana mjini, lakini kwa Kijana Kanizio kupita kwa barabara katika kijiji hiki ni fursa adhimu kwake.
Airtel Fursa umelenga katika kuwezesha vijana wajasiriamali hapa nchini kwa kutoa msaada kwa vijana ambao wanaonyesha juhudi ya kujikomboa na changamoto za maisha katika Jamii zinazowazunguka kwa kuwapatia vitendea kazi na kutoa mafunzo ya biashara ya ujasiriamali. Airtel Fursa ni moja ya sehemu ya utekelezaji wa wajibu wa Airtel katika kurudisha sehemu ya faida wanayoipata kwa jamii ili kukidhi matakwa ya kiuchumi, na kuunga mkono jitihada za serikali katika kubadilisha maisha ya wananchi.
Akiongea wakati wa makabidhiano afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki alisema kuwezeshwa kwa kijana huyu kupitia Airtel fursa ni ukombozi wa kiuchumi kwa familia yake na Jamii inayomzunguka. Kama alivyokuwa amebainisha katika maombi yake kupitia mpango wa Airtel Fursa, hatua hiyo imetafsiriwa kama kichocheo cha mapinduzi ya kibiashara na fursa za kiuchumi kijijini hapa Kumnazi.
“Tunawahimiza vijana kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa hizi pale zinapojitokeza kwani baadhi ya vijana wamekuwa wakihamia mijini na kuacha kazi ya uzalishaji mali kufanywa na wazee na wanawake na hivyo kukwamisha maendeleo vijijini” aliongeza Dangio
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Kanizio amesema msaada huo ni mkombozi wa maisha yake na familia huku dada yake Agnes Annatory akiishukuru Airtel kwa kuwa mkombozi kwao.
Kanizio alisema “ nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kufanikisha ndoto zangu kwa kuweza kunipatia vifaa hivi vya kisasa kwani nimekuwa nikipata ugumu wa kupata wateja kwani sikuwa na vitendea kazi vya kutosha vitakavyoweza kukidhi mahitaji ya wateja wangu, lakini sasa ninaamini nitapata Wateja wengi sana na kuinua biashara yangu.
Mpaka sasa Airtel Fursa toka ianze imeweza kuwainua vijana wapata 2800 kwa kuwapatia vifaa mbali mbali kwa kuendeleza bishara zao na vile vile kutoa mafunzo ya biashara katika mikoa mbali mbali hapa nchi, na katika msimu huu wa pili Airtel Fursa imetenga kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya kubadlisha maisha ya vijana hawa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.