Wanafunzi wa shule ya mloganzila wakiwa wanamsikiiza diwani huyo kabla ya kuzindua maradi wa maji. |
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE UTAIBADILISHA YA GAZETI HIYO
WANAFUNZI wa shue ya msingi mloganzila iliyopo kata ya kiluvya ’B’ Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani waliokuwa wamekithiri kwa tabia ya utoro kutokana na kukabiiwa na changamoto ya siku nyingi ya upatakanaji wa maji safi na salama kwa sasa wamepata mkombozi baada ya kukamilika kwa mradi wa maji ya bomba.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti shuleni hapo katika hafla fupi ya uzinduzi wa mradi huo wa maji wanafunzi hao walisema kwamba hapo awali walikuwa wanasoma katika wakati mgumu kutokana na kukosa kabisa huduma ya maji safi na salama ambayo ilikuwa inawapa shida pindi wanapopatwa na kiu au wakati wa kwenda kujisaidia.
Athanasi Joseph ambaye anasoma darasa la nne alisema kwamba kutokana na kuwepo kwa kero ya maji iliwalazimu wanafunzi wengine kuamua kutokwenda shule na wengine pindi wanapopata kiu kwenda kuomba maji kwa majirani na pindi wakikosa wanarudi nyumbani kabla ya vipindi vya masomo kumalizika.
Naye Neema Sangakero ambaye anasoma darasa a saba alisema kwamba tangu ajiunge na shule hiyo hajawahi kuona huduma yoyote ile ya maji hivyo wakati mwingine pindi wanapokwenda kujisaidia wanatumia makaratasi pamoja na magazeti katika kujisafisha kitu ambacho amedai ni hatari sana katika afya zao.
“Kwanza kabisa tunamshukuru diwani wetu wa kata ya Kiluvya kwa kuiona kero hii maana ni ya muda mrefu,kuhusu utoro kwa wanafunzi ni kweli kabisa tena wanafunzi wengine wanaamua kutokuja shuleni kabisa maana wakati mwingine tunapata kiu lakini maji hakuna kwa hiyo mtu anaamua asiche kabisa shuleni hivyo utoro uiongezeka lakini kwa maradi huu nadhani mtoro hautokuwepo tena ,”aisema Neema.
Kwa upande wake mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo ya Mloganzila Grace Msele amekiri kuwepo kwa hali hiyo ya kukithiri kwa utoro kwa wanafunzi wake katika siku za nyuma kutokana na kero ya kutokuwa na maji katika eneo hio hivyo kusababisha kupelekea baadhi ya wanafunzi kutohudhuria masomo darasani.
“kukamilika kwa mradi huu wa maji katika shule yetu ya mloganzila ni jambo kubwa la kumshukuru mungu, pamioja na diwani wetu wa kata ya Kiluvya ndugu Kitale kwani hapo awali mambo yalikuwa ni magumu sana kwa wanafunzi wetu kwani wakati mwingine wanatoroka madarasani kwenda kutafuta maji kwa majirani na wakiende hawarudi tena darasani hii hai iichangiwa na ukosefu wa maji,”alisema Grace.
Aidha Mwalimu Grace alisema kwamba kuwepo kwa tatizo la muda mrefu shuleni hapo la ukosefu wa maji pia liliweza kuwafanya wanafunzi kuwenda kujisaidia bila ya kutumia maji yoyote hivyo kuhatarisha usalama wa afya zao.
Akizungumzunguzia changamoto nyingine katika shule hiyo alisema kwa sasa kuna wanafunzi wengine wanakaa chini ukizingatia na mwaka huu wameshaandikisha idadi ya wanafunzi wa darasa la kwanza wapatao 273 hivyo kuwalazimu wengine kusoma katika mazingira magumu kutokana na kutokanana kuwepo kw auhaba wa madarasa pamoja na madawati.
“Kwa sasa shule yetu hii kwa kipindi cha mwaka wa 2016 tumepata idadai kubwa sana ya wanafunzi wadarasa la kwanza ni wengine sana wapo 273, hivyo wanasoma kwa shinda sana kwani madarasa amabyo yapo ni machache sana hivyo tumeamua wawe wanasoma kwa shifti wengine waingie asubuhi na wengine waingie mchana,”alisema.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya kiluvya (CHADEMA) Idan Kitale alisema kwamba aliweza kubaini chanagmoto ya maji katika shule hiyo baada ya kufanya ziara na kukuta wanafunzi wapo katika hali mbaya kutokana naa huduma ya maji wanakwenda kuipata kwa majirani hivyo akaamua kufanya harambee kwa wananachi kwa ajili ya mradi huo wa maji.
“Mimi baada ya kuchaguliwa kuwa diwani nilianza kwa kutembelea maeneo mabali mbali ikiwemo shule za sekondari na msingi lakii shule hii niliikuta ina tatizo kubwa la maji kwani tangu iipoanzishwa haijawahi kuwa na maji hivyo wanafunzi na walimu wao wnapata tabu sana katika maji ya kunywa na apindi wapokwenda kujisaidia maji nap hakuna kwa hiyo nikaona nilivalia njuga na nadhani limefanikiwa na mradi w maji nimeuzindua mimi mwenyewe na maji yameanza kutoka,” alisema Kitale.
Diwani huyo pia aliwataka wazazi pamoja na walimu kushirikiana katika mambo mbali mbai ya kimaendeleo na kwamba changamoto zote zinazowakabili ikiwemo madawati, madarasa, umeme, na mengineyo atazifanyia kazi kwa bidii ili kuweza kuleta ukombozi kwa wananchi wa kata ya Kilivya ambao walikuwa wameachwa kwa muda mrefu katika kupatiwa miradi ya maendeleo.
SHULE hiyo ya msingi ya mloganzila licha ya kukabiliwa na changamoto ya maji kwa kipindi kirefu bado pia bado wanafunzi wake wanasoma katika mazingira magumu kutokana na kukabiliwa na uhitaji mkubwa wa madawati 500 pamoja na madarasa 12.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.