Wananchi kwenye kusanyiko la hadhara lililofanyika katika viwanja vya stendi ya daladala. |
MBUNGE wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mbaula(CCM) amepiga marufuku watendaji wa mitaa na Kata zote kukusanya fedha kwa mamalishe ili kuwapeleka Hospitali kupimwa afya zao kabla ya kupewa vibali vya kufanya biashara pia watendaji wa mitaa na Kata hiyo kuwakamata watu walioanzisha machinjio bubu na kuunza nyama kwa wananchi isiyokaguliwa.
Mabula alitoa kauli hiyo jana wakati akihutubia mamia ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Kata za Kishiri na Igoma ikiwa ni ziara yake ya kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2015 uliomwezesha kushinda kuwa Mbunge wa Jimbo hilo.
Mbunge Mabula alianza mkutano wake kwa kutoa fursa kwa wananchi wenye maswali ya kero na changamoto zilizopo katika maeneo ya mitaa yao yakihusu sekta za Afya, Elimu, Miundombinu ya barabara, Ardhi, Uchumi, Maji na Umeme ili kuzitafutia ufumbuzi na majibu kutoka kwa wataalamu wa Kata na mengine kuyachukua ili kuyafikisha kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji hilo.
Awali Monica Masanja (35) mkazi wa mtaa wa Igoma mashariki alimuelezea Mbunge Mabula jinsi mamalishe wa maeneo ya Kata za Igoma na Kishiri kubugudhiwa kwa kutozwa fedha na Afisa Afya wa Kata kupitia watendaji wa mitaa ili wapimwe afya zao kabla ya kuanza shughuli zao jambo ambalo ni kero kwao.
Mabula akijibu hoja hiyo iliyoonekana kupigiwa kelele na wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo hasa mamalishe, alisema kuwa kwa kitendo cha watendaji na Afisa Afya wa Kata ya Igoma, Hussin Mjuba kuwakamata na kulazimisha kuwatoza fedha kwa madai ya kukusanja ili kuzipeleka hospitali ili wapewe huduma ya kupimwa afya zao kuwa hilo ni jibu na kuonya kuacha kufanya hivyo.
“Marufuku kuanzia leo kwa mtendaji wa Kata, Mitaa na mafisa afya kuwatoza fedha za kupimwa afya zao mamalishe hiyo si kazi yenu na mamalishe mnatakiwa kwenda Hosiptali kupimwa na kupewa majibu na daktari ambayo utakuwa nayo wakati wa kuomba au kufungua biashara yako ili afisa afya atakapokuuliza unampatia na si kutoa fedha kiasi cha Sh 50,000/= hiyo ni rushwa kataeni nendeni kwenye vituo vya Afya na Hospitali na kuchangia Sh 5,000/= tu mkipewa risti kisha mpate huduma na kuwasilisha kwa Afisa Afya wa Kata husika na si vinginevyo,”alisema.
Mabula pia amewataka Mtendaji wa Kata ya Igoma, Baruhan Awardh, Afisa Afya Mjuba na Afisa Mifugo wa Kata hiyo, Hussen Lugozi kuwachukulia hatua kali za kisheria watu aidha wafanyabiashara wa nyama kwa kuanzisha machinjio bubu na kuuza nyama isiyokaguliwa jambo ambalo ni kinyume na ukiukwaji wa sheria zilizopo ikiwemo taratibu za leseni za halmashauri ya Jiji pia wataalamu wa Kituo cha Afya Igoma na Zahanati wanaowafukuza wagonjwa wachunguzeni kisha tuwachukulie hatua.
“Kata ya Igoma na Kishiri zimeathiriwa na ugonjwa wa kipindupindu hiyvyo ni lazima tuchukue tahadhari za na kuchukua hatua kwa watu wanaokiuka utaratibu wa kisheria kujifanyia biashara kama hiyo ya machinjio bubu na kuendelea na kufuga mifugo kama ng’ombe, mbuzi, nguruwe, kondoo kwenye makazi ya watu jambo ambalo wananchi wameendelea kulalamika katika hoja zao hapa hivyo chukueni hatua,”alisisitiza.
Mabula pia aliwaeleza wananchi katika mkutano huo kwamba wanaendelea na mkakati wa kuiboresha Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana iliyopo eneo la Kata ya Butimba ambapo kwa mwaka huu wa fedha 2016/2017 tunataraji kujengwa jengo la Wodi ya wanaume na vyumba vine vya madaktari ili kuwezesha kutoa huduma katika mazingira mazuri pia kuweka X-Ray na Atrasound ili kuwezesha vipimo hivyo kutoa huduma Hospitalini hapo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.