Na PETER FABIAN, MWANZA.
HALMASHAURI Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana kwa niaba ya Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya hiyo wamemchagua kwa kishindo, Kada Jamal Abdul “Babu” kuwa Mjumbe wa mpya wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho taifa (NEC) wilayani hiyo.
Abdul “ Babu” alichaguliwa jana na wajumbe wa Mkutano maalum wa Halmashauri kuu kwa niaba ya Mkutano Mkuu wa Chama hicho Wilaya kwa mujibu wa Katiba ya CCM toleo la 2012 kujaza nafasi iliyoachwa na aliyekuwa MNEC wake, Laurency Masha, aliyekihama Chama hicho na kutimkia kujiunga na Chama cha Damokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mwishoni mwa mwaka jana.
Mgeni rasmi na msimamizi wa uchaguzi huo, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, awali akiwahutubia wajumbe aliwahasa kutokuwa wanafiki na kuendeleza makundi na kuwachonganisha wagombea wanaoshinda dhidi ya walioshindwa kwa wanachama na viongozi hasa baada ya chaguzi kumalizika ikiwemo huo wa kujaza nafasi ya Mjumbe wa NEC taifa kutokea Wilaya ya Nyamagana.
“Niwaombeni sana wagombea tunapoingia kwenye uchaguzi wowote ule tuwe wamoja na hata baada ya uchaguzi kumalizika na mshindi kupatikana tuendelee kuwa wamoja na kushirikiana ili Chama kiendelee kutekeleza majukumu ya kuwatumikia wanachama wake na wananchi ili serikali itekeleze Ilani kwa vitendo ikiwemo kushughulikia changamoto na kero mbalimbali kwenye maeneo yetu,”alisisitiza.
Mtaturu akitangaza matokeo ya uchaguzi huo baada ya kura kupigwa, aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa wajumbe waliohudhulia walikuwa 104 lakini waliopiga kura ni 101 ambazo ni kura halali na hakuna kura iliyoaribika, mgombea Dr Sillinus Nyanda alipata kura 1, Patrick Kambarage kura 9, Kelebe Luteli kura 12 na Jamal Abdul “Babu” akishinda kwa kupata kura 79 na kuwa MNEC.
Kwa upande wake MNEC aliyechaguliwa kwa kishindo, Abdul “Babu” aliwashukuru wajumbe na wote wa mkutano huo kwa kumpatia lidha hiyo pia kuwapongeza wagombea wenzake aliowashinda na kuwaahidi na kuomba ushirikiano wa kukiimarisha Chama hicho kuanzia ngazi ya matawi, kata na wilaya, ambapo alianza majukumu yake kwa kwenda kutembelewa wagonjwa Hospitali ya Rufaa Bugando (MBC) akiwemo kumuona Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Mkuyuni ,Wambura Kitati .
“Tuendelee kuwa wamoja kama ambavyo kila mmoja alikuwa akitafuta nafasi hii, pili tushirikiane wote kuhakikisha CCM Nyamagana inaendelea kuwa mshindi katika Chaguzi za kiserikali za Wabunge, Madiwani na Wenyeviti wa Mitaa, pia sitombagua mtu na zaidi naomba ushirikiano wenu na lililopo ni kuwatumikia wanachama wote bila ubaguzi pamoja na wananchi wa Wilaya hii, Alisema.”.
Abdul aliwaeleza wajumbe na viongozi wa mkutano huo kuwa amejipanga kusaidiana na wanachama wote kuendeleza mazuri ya CCM pamoja na kuwa mwakilishi ambaye hata kuwa chanzo cha kupokea na kulea hoja za kuzalisha makundi na migogoro baina ya viongozi na wanachama ngazi za matawi, kata, wilaya na mkoa kwa ujumla hivyo ni vyma wanachama na viongozi wakajenga utamaduni wa kuwa watumishi wenye sifa na ubunifu wa kukisaidia Chama ili kiendelee kushinda na kuunda serikali kila chaguzi zinapotokea.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Raphael Shilatu, aliwapongeza wajumbe hao na kusisitiza kauli ya Katibu Mtaturu ya wanachama kutokuwa chanzo cha kuwachochea wagombea na kuwa chanzo cha kuibua makundi na migogoro baina ya viongozi na wanachama jambo ambalo kwa sasa lisipewe nafasi hiyo
Shilatu aliwaomba viongozi wa Kata na Matawi kuanza mchakato wa kujaza nafasi za viongozi ambao hawapo katika nafasi zao kutokana na sababu mbalimbali badala ya kung'ang'ania kuwa makaimu katika nafasi hizo ili kuwapa nafasi wanachama kujitokeza kuomba kugombea ili kujaza nafasi hizo kwa lengo la kuwatumikia wanachama na wananchi katika maeneo yao, kwa kuzingati Katiba na taratibu za Chama hicho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.