ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 19, 2016

ETIHAD YAPEWA TUZO YA SHIRIKA LA NDEGE LA MWAKA 2016 NA JARIDA LA AIR TRANSPORT WORLD

Viongozi kutoka shirika la Ndege la Etihad wakiwa na tuzo ya shirika la Ndege la mwaka 2016 waliyopokea kutoka jarida la Air Transport World (ATW) katika hafla iliyofanyika nchini Singapore. Kutoka kushoto Hareb Al Muhairy, Makamu wa Rais masuala ya kishirika na kimataifa; Karen Walker, Mhariri mkuu wa jarida la ATW; James Hogan, Rais na Afisa mtendaji; na  James Rigney, Afisa mkuu wa Fedha.

 PRESS RELEASE
Shirika la Ndege la Etihad limetunukiwa tuzo ya Shirika la Ndege la mwaka 2016 kutoka Jarida kubwa la Air Transport World (ATW) lililopo nchini Marekani linaloandika habari za usafiri wa anga. Tuzo hii imelitambua Shirika hili kwa kuwa na timu iliyo na mikakati inayohamasisha ukuaji wa Shirika na kukuza ushikiano wake wa kipekee; katika kuleta bidhaa zenye manufaa makubwa; kujenga nguvu kazi yenye hamasa; na kujenga utetezi wa kidiplomasia wakati wa ugomvi mkali kati yao na wasafirishaji wa Wamarekani. 

Shirika la Ndege la Etihad lilichaguliwa na bodi ya wahariri wa jarida hili huku kukiwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mashirika zaidi ya 100 kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni. Tuzo hii ilitolewa katika hafla ya chakula cha jioni iliyohudhuriwa na wadau wa sekta ya usafiri wa anga. Shughuli hii huandaliwa mara moja kila mwaka, ya mwaka huu ikiwa ya 42 tangu kuanzishwa kwake na kufanyika usiku wa kuamkia tamasha la anga la Singapore.

James Hogan, Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Etihad, alisema: “Tuzo hii ni kiashiria cha kufikia malengo tuliyojiwekea takribani miaka 13 iliyopita ya kuwa salama, kuwa shirika lenye faida na kuwa shirika lenye ubora wa hali ya juu. Inaonyesha nguvu zetu - mbinu imara za biashara, bidhaa zenye ubunifu na huduma iliyo bora zaidi inayotolewa na wafanyakazi zaidi ya 27,000 walio na ari kubwa. Nimefurahi kupokea zawadi hii kwa niaba yao, kama Shirika, tumejitahidi kutoa huduma za kipekee kwa wasafiri na tumekuza biashara yetu ili kusaidia sura ya usafiri wa anga duniani”.

Ili kustahili hii tuzo, ATW walisema Shirika lilitakiwa kuonyesha mafanikio ya kipekee katika operesheni zake, uwezo wa kifedha, huduma bora kwa wateja, usalama na mahusiano bora ya wafanyakazi. Timu ya uongozi wa juu pia ilibidi kuonyesha ubunifu na uwezo wa kuvumbua mikakati itakayoipa kampuni muonekano tofauti na nyingine.

Karen Walker, Mhariri Mkuu wa jarida la Air Transport World, alisema: “Shirika la Ndege la Etihad limejitenga na wengine na linaenda katika mkondo wake wakipekee. Tunayo furaha kusherekea mafanikio ya timu ya Etihad katika tuzo za mwaka huu za ATW hapa Singapore. “Etihad inastahili kupewa tuzo hii ya juu ya Shirika la Ndege la Mwaka”, alisema James Hogan huku akisisitiza kuwa “Suala sio kuwa shirika kubwa tu bali shirika bora zaidi”
·         Kwa upande wa bidhaa na huduma kwa wateja, Shirika la Ndege la Etihad lilielezewa na ATW kuwa wabunifu, wakiweka msisitizo katika vyumba vyao vya kipekee ndani ya Airbus A380 na Boeing 787. Pia waliiongelea “Makazi” ambayo ni vyumba vya kwanza duniani kuwa na sehemu tatu za; kulala, kupumzika na bafu.
·         Katika mahusiano ya kibiashara, ATW waliona Etihad na washirika wametengeneza mtandao wenye faida duniani kama msingi wa mbinu zake kibiashara. Ushirikiano wake na airberlin, Darwin Airline (iliyopo Uswisi), Air Serbia, Alitalia, Jet Airways, Air Seychelles na Virgin Australia umesaidia Shirika kuwapa wateja wao chaguo zaidi, uwezo wa kujadili bei na wasambazaji, mafunzo kwa wafanyakazi na mtandao uliosambaa zaidi ulimwenguni.
·         Katika mgogoro kati ya Etihad na wasafirishaji wa Marekani juu ya vitendo visivyohamasisha ushindani; ATW walisema James Hogan na timu yake walionyesha staha na heshima kwa kulitetea Shirika lao na mbuni zake kwa ukweli kuliko kutumia mashambulizi. Wahariri wa ATW walimwaga sifa kwa Etihad ambapo James Hogan alisema: “Mawe mengi yamerushwa kwetu, lakini tumejibu kiutulivu na kwa ukweli, tulionyesha ushindani mpya tulioleta katika soko.”
·         Upande wa wafanyakazi, ATW iliwaelezea Etihad kama “raia mwema” ikilielezea nguvukazi yao kama ‘familia’ na kwa kufanyia kazi mikakati yao ya kukuza nguvukazi yao (ikiwa na raia 3,000 wa UAE) na kuwapa kazi kupitia programu mbalimbali. Wafanyakazi wanaungwa mkono na Maafisa rasilimali, timu ya ustawi, wakipata huduma mbalimbali kama sehemu za mazoezi, sehemu nzuri za malazi na chekechea kwa watoto wao.
·         Katika mipango endelevu, ATW iliwapongeza Etihad kwa mipango yake ya kupunguza matumizi ya mafuta, kufanya utafiti wa nishati mbadala na washirika wake wakuu, na kuwashughulisha wafanyakazi katika programu za kuokoa mazingira.
Katika mwaka 2015, Shirika la Ndege la Etihad lilizindua njia sita zaidi katika mabara 3 na hivyo kufikisha jumla ya vituo vyake ulimwenguni kufika 116 kwa kutumia ndege 121. Zaidi ya wageni milioni 17 wamesafiri na Shirika hili mpaka mwaka jana, kutoka milioni 15 wa mwaka 2014. Etihad ilizindua ndege yake mpya aina ya Boeing 787 Dreamliner – ya kwanza kati ya 71 zilizowekwa oda. Shirika la Etihad lilitambuliwa na bodi ya wahariri wa ATW kwa “kuwa na ukuaji wa haraka na uliopangwa, kutoa huduma bora na zinazofikia malengo yao na kwa kuwa na fikra endelevu daima”. Etihad pia ilisifiwa kwa “kuwa na uwezo mzuri kifedha, usalama na uwezo wake kubeba mizigo” 
ATW ni jarida la kimamlaka linalotoka kila mwezi na kukidhi mahitaji ya jumuiya za wadau wa usafiri wa anga ulimwenguni. Wahariri wake wameteuliwa kutoka kila tuzo za uandishi wa usafiri wa anga zilizopo, wakiangalia uzoefu na utaalamu wao.

Tuzo za mafanikio katika sekta ya anga za ATW zilianzishwa 1974 ili kutambua umahiri katika operesheni za mashirika ya ndege duniani na kuwapa pongezi wadau wa sekta hiyo. Jarida hili lipo Marekani na timu yake ya wahariri imefika kote ullimwenguni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.