ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 22, 2016

AIRTEL YAMWAGA MILIONI 10 KWA MJASILIAMALI KUOKOA MAZINGIRA.

Mjasiliamali Amina Iddi (20) (kulia ) akijaribu moja ya vifaa alivyokabidhiwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa wa kuwezesha vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 24 akizungusha mashine ya kutengenezea majiko sanifu baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo vyenye thamani ya sh10 Mil kijijini kwao Magole mtaa wa Chabwanga wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro jana.
Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi akimkabidhi kijana Amina Iddi (20) sehemu ya vifaa vya kutengenezea majiko sanifu vyenye thamani ya sh 10 Mil baada ya kuwezeshwa na mpango wa Airtel Fursa katika hafla iliyofanyika nyumbani kwao katika  kijiji cha Magole mtaa wa Chabwanga wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro. Kulia ni mama wa Amina, Asia Juma (50) na kushoto ni afisa mauzo wa Airtel Aminata Keita.
Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi  akionyesha moja ya jiko sanifu ambalo bado halijakamili yanayoandaliwa na mjasiliamali Amina Iddi (20)wa tatu kulia baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa katika hafla iliyofanyika nyumbani kwao katika  kijiji cha Magole mtaa wa Chabwanga wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Airtel yawezesha uzalishaji wa Majiko sanifu  kuokoa Mazingira mkoani Morogoro

·       Airtel  Fursa yamwaga milioni 10 kwa mjasiliamali kuokoa Mazingira

Kampuni ya simu  mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa kusaidia jamii wa Airtel FURSA imekabidhi vifaa mbalimbali vya ufundi vyenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa mjasiliamali Amina Iddi wa kijiji cha Magole mtaa wa Chabwanga-Magole Mkoani Morogoro. Uwezeshaji huo kupitia Airtel FURSA ni kwa ajili ya kutengeneza majiko sanifu maarufu kama jiko matawi  ili kusaidia pia kutunza mazingira ya kijiji hicho na mkoa kwa ujumla .

Kijiji cha Magole mkoani Morogoro kinakadiriwa kuwa na takribani wakazi kati ya 1500 na zaidi ambapo shughuli zao kubwa za uchumi ni kilimo cha mazao ya chakula kama Mahindi, Maharagwe na Mpunga.

Mama mzazi wa Amina Iddi, Asia Juma (50)alieleza kufurahishwa na kitendo cha mwanae kupata msaada huo wa vifaa na malighafi zake kwa ajili ya majiko hayo yenye kubana matumizi na rafiki kwa mazingira.Majiko matawi yana uwezo wa kutumia mkaa na kuni chache huku yakiwa na sifa ya kuhifadhi joto kwa muda mrefu sambamba na kutoa moshi mchache.

Tunashukuru kwa msaada huu wa vifaa vitakavyomwezesha Amina kuendelea na shughuli zake za ujasiliamali, Amina anabidii na jitihada za hata kutoa ujuzi kwa vijana wenzie . Wingi wa majiko matawi itasaidia   kuokoa mazingiza ya kijiji.

Kwa upande wake Bi, Amina Iddi (20) baada ya kukabidhiwa vifaa  hivyo alieleza kufurahishwa na mpango wa kampuni ya Airtel kupitia Airtel FURSA kwa jitiada zake za kuwawezesha vijana wajasiriamali katika nyanja mbalimbali za kuzalishaji mali.

“ndoto yangu sasa imetimia baada ya kupata vifaa hivi, vitaniongezea uzalishaji na utengenezaji wa majiko sanifu na kunipa chachu ya kuwa mbunifu zaidi. Sasa nina uwezo wa kutengeneza majiko sanifu kati ya 10 hadi 15 kwa siku, kabla ya hapo manunuzi ya vifaa hivi, yalinikwamisha na gharama zilikua juu jiko moja lilikuwa linagharimu kiasi cha sh14,000 baada ya kununua vipuli na kuuza kwa wateja kati ya sh18,000 hadi sh 25,000  lakini kwa sasa baada ya kupata vifaa hivi vitasaidia kuondokana na gharama za pesa za kununua vifaa, pia nitayauza kwa bei nafuu kwa wakazi wa hapa kijijini”.alisema Amina.

Meneja wa Mradi wa jamii wa Airtel Fursa Bi, Hawa Bayumi alisema kuwa “Airtel FURSA imelenga kuwawezesha vijana wajasiliamali wenye malengo ya ubunifu kama Amina leo ili kukuza biashara zao na kuleta ubunifu kwa faida ya jamii nzima.

Bayumi alieleza “Airtel FURSA mwaka huu ipo katika msimu wa pili na imetenga jumla ya bilioni 1 kwaajili ya wajasiliamali nchi nzima, ndani ya mizezi mitatu tayari imeshawaguza vijana 600 kwa kuwapatia elimu ya ujasiliamali na wengine 14 kufaidika na msaada wa vifaa vya kutendea kazi ambapo mkoa wa Morogoro umefaidika kupitia kuwezesha kwa wajasiliamali, Amina Iddy (20) kutoka kijiji cha Magole wilaya ya Kilosa na Hashimu Mikidadi wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro vijijini.

“Tunajivunia vijana wa Mkoa wa Morogoro waliooonyesha uthubutu kama Amina na Hashimu ambaye yeye alipata fedha zilizotumika katika ukarabati wa bucha ya nyama na vifaa ikiwemo majokofu ya kuhifadhia nyama ikiwa na thamani ya sh9 Mil wakati Amina amepatiwa vifaa vya kutengeneza majiko safuni vyenye thamani ya sh10 Mil”.alisema Bayumi.

Mwisho

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.