NA VICTOR MASANGU,PWANI
MKUU wa Mkoa wa Pwani injinia Evarist Ndikilo ametoa muda wa siku saba kwa watendaji wa mitaa, watendaji wa kata,pamoja na wazazi wote wenye watoto wao ambao wamefanikiwa kufaulu kuingia kidato cha kwanza lakini mpaka sasa wameshindwa kuwapeleka wanafunzi hao licha ya serikali kuagiza elimu kutolewa bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne.
Injinia Ndikilo ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya siku moja katika Halmashauri ya mji wa Kibaha ambapo ameweza kuzungumza na watumishi na watendaji mbali mbali wa serikali na vyama vya siasa aambapo amesema kuwa suala hilo atalivalia njuga na mzazi ambaye atakaidi agizo hilo atapelekwa katika vyombo vya dola.
Ndikilo alisikitishwa kuona baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani kuna wanafunzi wamefaulu na kupata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza lakini mpaka sasa bado wamekaa majumbani kwao bila kuripoti shuleni.
Alisema kwa sasa serikali ya awamu ya tano ilishasema elimu ni bure hivyo wazazi wanatakiwa kuacahna na visingizio vya aina yoyote vile juu ya suala la kutompeleka motto shuleni wakati amefaulu na nafasi ameipata hivyo asingependa kuona hali hiyo inakuwepo katika Mkoa wa Pwani.
“Kwa hili ndugu zangu siwezi kulivulimia hata kidogo kwa hiyo nawaagiza watendaji wote wa mitaa, watendaji wa kata pamoja na wazazi wote wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha sasa wanafanya jitihada za makusudi kuwapeleka watoto wao ambao wamepata nafasi ya kujiunga na akidato cha kwanza kwani elimu ni bure na mimi ili nitalifuatilia kwa ukaribu,alisema Ndikilo.
Aidha alifafanua kwamba katika awamu hii ya tano ya uongozi wa Rais wa John Magufuli haitaki kuona watendaji wanakuwa wazembe na hawatimizi majukumu yao ipasavyo hivyo wanapaswa wachape kazi kwa bidii ili kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo .
Akizungumzia suala la dhana ya elimu bure kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari amebainisha kuwa serikali ya Mkoa wa Pwanikwa sasa tayari imepokea kiasi cha shilingi milioni 579 na kutoa angalizo kwa watendaji kuachana na tabia ya kuzihujumu fedha hizo zilizotolewa atawawajibisha bila na kuwachukulia hatua.
“Hizi fedha ambazo zimetolewa nataka situmike kama jinis zilivyopangwa sitapenda kuona mtumishi wa serikali au mtu yoyote amehusika katika ubadhirifu wowote ule fedha zote ziwafikie walengwa na sio zitumike katika kazi nyingine ili kwa kweli naomba sana mlizingatie maana Rais ataki mchezo kabisa na fedha hizi na atakaebainika kazi ajifukuzishe yeye mwenyewe,” alifafanau Ndikilo.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Hajat Halima Kihemba akitoa taarifa fupi kuhusina na sekta ya elimu katika Wilaya yake alisema bado kuna changamoto kwa baadhi ya shule kutokuwa na maabara, matundu ya vyoo, sambamba na viti vya kukalia hivyo kunahitajika nguvu ya ziada katika kulitilia mkazo suala hilo.
Kwa upande wake mmoja wa wazazi aliyejitambulisha kwa jina la Method Mselewa ambaye ni mkazi wa Wilayani Kibaha alisema kwamba wazazi wanatakiwa kulitekeleza agizo hilo lililotoewa na Mkuu wa Mkoa wa pwani la kuwapeleka watoto wote waliopata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza.
Halmashauri ya mji wa kibaha imeshika nafasi ya pili katika Ngazi ya Mkoa wa Pwani katika matokeo ya kidato cha kwanza ambapo mpaka sasa wanafunzi walioripoti kwa sasa ni asilimia 70.4 huku asilimia 29.6 bado wakiwa hawajaripoti mashuleni.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.