NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
WANANCHI wa eneo la mtaa wa Picha ya ndege Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani wamegomea kulipia ongezeko la kodi ya majengo kutokana na kuongezewa kodi hiyo kwa kiwango kikubwa kutoka kiasi cha shilingi elfu kumi mpaka shilingi elfu hamsini na zaidi bila ya wao kushirikishwa na watendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha kitu ambacho ni kinyume cha taratibu.
Wakizungumza katika mkutano huo wa adhara ulioandaliwa kwa lengo la kuweza kujadili changamoto mbali mbali zinazowawakabili ikiwemo suala hio la kodi wananchi hao wameshangazwa kwa kitendo hicho cha Halmashauri kuanza kuwalipisha kodi mpya ya majengo kinyume cha taratibu na kanuni zilizowekwa.
Wananchi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti akiwemo Godfrey Mwaipopo, , Nassoro Juma, Seleman Kiwango na Raumo Mrema walisema mesema kwamba hapo awali kodi ya majengo kima cha chini walikuwa wanalipa kiasi cha shilingi elfu kumi tu lakini kwa sasa wanapaswa kulipia shiingi elfu hamsini mpaka shilingi elfu sabini kitu ambacho wamekipinga kutokana na kodi hiyo sio rafiki kwao na inawakandamiza.
Mmoja wa wananchi hao Godfrey Mwaipopo alisema kwamba wanashangazwa na watendaji wa halmashauri ya mji wa kibaha kufanya mambo kiunyume na taratibu zilizowekwa kwa kuwapandishia kodi ya majengo kitu ambacho amedai ni kunyanyasana na kuwa hawawezi kulipa kodi hiyo.
“Sisi wananchi wa mtaa wa picha ya ndege tunaonewa sana maana hapo awali sisi tulipata hati ya ulipaji mzuri kwa kuongoza kulipa kodi, hii leo tunashangaa kodi inapandhindishwa kiholela tena ahata sisis wananchi hatujashirikisha kabisa ni kitu cha ajabu sana lakini sisi kwa kifupi hii kodi hatulipi hata watupeeke mahakamani,” alisema Mwaipopo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya mjin wa Sanifodi Mlowe alisema kwamba malalamiko ya wananchi hao wa mtaa ya picha ya ndege tayari ameshayasikiahivyo suala hilo atahakikisha analivalia njuga ila wanaanchi hao wasiweze kuonewa na kupata haki yao stahiki.
Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba upandishwaji wa kodi hiyo ya majengo ulifanyika wakati baraza la madiwani lililopita tayari likuwa limeshamaliza muda wake hivyo kama kuna watendaji waliamua kufanya hivyo ni kinyume cha taratibu na kwamba atalifanyia kazi mapema iwezekanavyo ili kweza kuangalia upya ongezeko hilo.
“Kwa kweli kilio hiki hata mimi mwenyewe kama mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa kibaha nilikisikia na mimi hapa ninawaahidi kuwa ni lazima nitalifanyia kazi kwani hili jambo naweza kusema limefanyika wakati baraza la madiwani lilikuwa tayari limevinjwa kwa hiyo nina imani baada ya muda mfupi japo ili litawekwa sawa,” alisema Mlowe.
Kwa upande wake Waziri na Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi akijibu malalamiko hayo ya wananchi alisema kwamba kitendo cha kuwalipisha kodi kubwa wananchi hao ni uonevu mkubwa na suala hilo atahakikisha analifuatilia kwa kina na watendaji watakaobainika wanafanya kazi kwa matakwa yao atawachukulia hatua.
Waziri Lukuvi alisema kwamba haiwezekani mwanananchi wa kawaida hata eneo lake halina hati ya nyumba lakini utakuta anatozwa kodi kubwa ya majengo tofauti na utaratibu ambao umewekwa hivyo Wizara yake suala hilo haiwezi kulifumbia macho hata kidogo.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hiziuliweza kubaini kwamba upangwaji wa ongezeko la kodi hizo za majengo umefanywa na baadhi ya watumishi wachache wa halmashauri ya mji wa kibaha pindi baraza la madiwani lilipovunjwa kwa maslahi yao binafsi bila ya kuzingatia miongozo na sheria zilizowekwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.