NA VICTOR MASANGU, PWANI
SHULE ya msingi ya mkoani iliyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani kwa sasa inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa madawati, madarasa pamoja na miundombinu ya madarasa kuwa mibovu na vyoo kuwa na nyufa hali ambayo inatishia usalama wa maisha yao kutokana na mazingira wanayosemea ni hatarishi na sio rafika kwao.
Hali hiyo imebainika baada ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikio kufanya ziara ya kushitukiza katika shule hiyo na kuweza kujionea ubovu wa majengo hayo wanayoyatumia katika shule hiyo kuwa ni chakavu kutokana na kutofanyiwa ukarabati kwa kipindi kirefu.
Mkuu wa shule hiyo Pregua Mseja amekiri kuwepo kwa hali hiyo ambapo alisema kwamba licha ya shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya ubovu wa miundombini lakini bado inakabiliwa na uhaba wa madawati pamoja na nyumba sita vya madarasa vina vuja maji kutokana na mapaa yake kutoboka hivyo wanafunzi wananyeshewa na mvua.
“Kwa sasa Mkuu wa Mkoa shule hii ina changamoto nyingi sana kwani licha ya ubovy wa majengo pamoja na vyoo bado mambo ya msingi yanahitajika kwa shule hii ili wanafunzi waweze kujisomea katika mazingira mazuri kwa mfano sasa kuna madasara sita ambayo yanavuja kweli wanafunzi wananyeshewa na mvua,” alisema Mseja.
Akizungumzia kuhusiana na fedha ambazo tayari wameshakwisha zipokea katika shule hiyo kutoka serikalini kwa ajili ya uendeshaji wa elimu bure alisema kwamba wameshapokea kiasi cha shilingi laki 437 ambazo zitatumika katika mahitaji mbali mbali ikiwemo suala la utawala michezo pamoja na mahitaji mengine ya msingi.
Baada ya Mkuu wa Mkoa kumaliza kufanya ukaguzi katika maejengo ya utawala, madarasa ya wanafunzi pamoja na kutembelea vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi hao alitoa agizo kwa halmashauri ya mji wa Kibaha kuhakikisha wanatafuta fedha haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kukarabati miundombinu hiyo ili kuwatendea haki ya msingi watoto hao.
Ndikiro alisema kuwa majengo hayo yanatakiwa kufanyiwa ukarabati wa haraka na kwamba halmashauri ya mji wa Kibaha ihakikishe inatafuta fedha ambazo zitaweza kusaidia katika kukarabati miundombinu hiyo ya majengo ili watoto waweze kujisomea katika mazingira mazuri.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kibaha Mauld Bundala aliunga mkono kauli ya Mkuu wa Mkoa ambapo alisema anaskitishwa sana na kuona wanafunzi wnasoma katika majengo amabyo yana nyufa kwani kunaweza kupelekea watoto hao kuangukiwa na majengo.
Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kibaha Grory Diamunye ambao nao walikuwepo katika ziara hiyo alisema atalivalia njuga suala hilo na kuahidi kulishughulikia haraka sana ili wanafunzi hao waweze kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki kwao kwani kufanya hivyo kutaweza kuwafanya waongeze hata kiwango cha ufaulu.
Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 764 kwa sasa bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madawati, madarasa, matundu ya vyoo, uchakavu wa miundombinu ya majengo ahali mbayo inwapa wakati mgumu wanafunzi hao kusoma katika mazingira ambayo ni hatari kwa masiha yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.