ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 18, 2016

HALI TETE MKWAJUNI JIJINI DAR ES SALAAM

Muda mchache uliopita GSengo BLOG imepokea taarifa hii na picha toka kwa mdau aliye eneo la tukio, zikitiririka kuwa  "Wananchi wa bonde la Mkwajuni Kinondoni wamefunga barabara ya Kawawa. Wanachoma matairi na kujaza magogo barabarani. Kama kuna mtu anakwenda Kinondoni kutokea Magomeni ama anakwenda Magomeni kutokea Kinondoni asitumie barabara ya Kawawa (kwa wenye magari)"

Kwa ufupi udadisi juu ya hatua hiyo imekuja kufuatia zoezi la Bomoabomoa ambapo leo lilikua likiendelea katika eneo la Mkwajuni, Dar es salaam, lakini safari hii wananchi waliobomolewa nyumba zao wameonekana kupandwa na hasira na kufunga barabara.

Wananchi hao wameamua kuchoma matairi katikati ya barabara na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo hadi askari wa FFU walipoingilia kati. 
TUTAENDELEA KUKUPA TAARIFA ZAIDI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.