ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 12, 2016

UHURU MAANA YAKE NI NINII? SHEIKH ABEID AMANI KARUME

Wakati Zanzibar ikiwa katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi yake yaliyoiondoa madarakani Serikali ya Zanzibar iliyokaa madarakani siku chache. Mapinduzi yaliyofanyika Januari 12,1964. 

Huku ikiwa katika mkwamo mkubwa wa kisiasa uliotokana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, 2015. Viongozi wa CUF wamesusia sherehe hizo.

Wakati Chama cha Mapinduzi (CCM) ikitaka uchaguzi urudiwe na Chama cha Wananchi (CUF) kinataka matokeo ya uchaguzi yatangazwe na mshindi wa urais atangazwe na kushika madaraka.

Yote Tisa tukiwa tunaomba kheri na kuwatakia mema kuwa muafaka upatikane, Hebu turudi nyuma na kumsikiliza mmoja kati ya waasisi wa Taifa hili la Tanzania ambaye alikuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume alizungumza vipi kuhusu maana ya UHURU. (BOFYA VIDEO)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.