ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 28, 2016

SUMATRA YATAKIWA KUINGILIA KATI MGOMO WA MASLAHI KATI YA MADEREVA WA DALADALA DHIDI YA MADEREVA WA TAX MWANZA.

MAMLAKA ya udhibiti wa vyombo vya nchi kavu na Majini (Sumatra), imetakiwa kuingilia kati Mgomo wa wa maslahi kati ya Mareva wa Daladala dhidi ya Madereva Texi, ili kuepusha adha ya usafiri inayowakabili Wananchi, wakiwemo akina mama wajawazito na wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali ya rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.
Ni mgomo Dalala zinazofanya safari zake kati ya Mwanza Mjini, Bugando na Bugarika uliodumu takribani saa tisa, huku sababu za mgomo huo zikieleza kuwa Madereva wa Daladala wanachukizwa na kitendo cha Texi kubeba abiria kwa bei ya shilingi mia nne, sawa na bei ya usafri wa daladala, jambo wanalodai kuwa linawakosesha mapato.
Mwenyekiti wa Chama cha Madereva mkoa wa Mwanza Dede Petro anasema kutokana na mgomo huo, vyombo vinavyohusika havina budi kulipa uzito tatizo hilo kwa kuwa linaathiri Wananchi, na kwamba viwango vya ulipaji wa kodi za ubebaji wa abiria havina budi kuwekwa katika uwiano unaolingana na Mamlaka zinazohusika.
Wakati hatima ya tatizo hilo ikiwa bado haijapatiwa ufumbuzi wa kudumu, Channel Ten ikalazimika kuwatafuta watendaji wa Mamlaka ya udhibiti wa vyombo vya nchi kavu na Majini (Sumatra) mkoa wa Mwanza, ili waweze kulizungumzia suala hilo lakini baadhi ya Maafisa wake waliofika katika eneo la mgomo huo, hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.