ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 1, 2016

KAGAME ATANGAZA KUWANIA MUHULA WA TATU.

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametangaza kwamba atawania urais kwa muhula wa tatu baada ya muhula wake wa sasa kumalizika 2017.
Kiongozi huyo alitoa tangazo hilo kwenye ujumbe wake wa mwaka mpya mnamo Ijumaa.
"Mumeniomba niongoze nchi hadi baada ya 2017. Kwa kuzingatia umuhimu wa hili kwenu, sina budi ila kukubali,” alisema Bw Kahame kwenye ujumbe wake uliopeperushwa moja kwa moja kupitia runinga.
Hata hivyo aliongeza kwamba hakusudii kuongoza Rwanda hadi kufa kwake.
Hii ni siku chache baada ya kufanyika asilimia 98 ya Wanyarwanda kuidhinisha marekebisho ya katiba ya kumruhusu Bw Kagame kuwania tena.
Kura hiyo ilifanyika mwezi uliopita.
Mabadiliko hayo, ambayo yanamuwezesha kiongozi huyo kutawala hadi mwaka 2034 imeshutumiwa na Marekani na mataifa mengine ya magharibi.
Kagame alianza kuongoza Rwanda kama rais 2000 baada ya kuwa na mamlaka makuu tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Amesifiwa kwa kurejesha uthabiti katika taifa hilo na kuendeleza ukuaji wa kiuchumi baada ya mauaji hayo.
Lakini wakosoaji wake wanasema yeye ni kiongozi wa kiimla ambaye huwa hawavumilii wapinzani. Ametuhumiwa pia kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu, madai ambayo amekanusha.CHANZO BBC SWAHILI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.