Twanga
pepeta kuwapagawisha uzinduzi wa Kibaha carnival ijumaa
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
BENDI kongwe ya muziki wa dansi hapa nchini Twanga Pepeta ‘wazee wa visigino’wanatarajia
kutoa burudani ya aina yake katika uzinduzi rasmi wa eneo jipya linalojulikana kwa jina la ‘Kibaha Carnival’ siku
ya ijumaa Desemba 4 mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi i wa habari hizi Katibu wa kamati
ya maandalizi kwa ajili ya siku hiyo
shauri Yomba Yomba alisema kwamba maandalizi kwa ajili ya aonyesho hilo
ya aina yake ambalo litakwenda sambamba
na huo yamekamilika.
Yomba yomba alisema kwamba katika uzinduzi huo utakuwa wa
aina yake kutokana na maandalizi mazuri ambayo tayari yamekamilika na baadhi ya
vitu vichache vinaendelea kufanyiwa kazi ili siku hiyo iwe ya kiutofauti zaidi.
“Hapa kikubwa ndugu mwandishi siku ya ijumaa desemba 4
nadhani itakuwa ni siku ya kipekee zaidi kwani ndio ile siku ambayo ilikuwa
inasubiriwa kwa hamu na shauku kubwa na mashabiki wa burudani pamoja na
kujionea eneo jipya la kisasa la Kibaha Carnival likizinduliwa rasmi hivyo
mambo yanakwenda vizuri mpaka sasa,”alisema Yomba Yomba.
Pia alibainisha kwamba siku hiyo ya uzinduzi mbali na bendi
ya Twanga pepeta kutakuwepo na burudani nyingine ambazo zitakuwepo na lengo kuu
ni kuhakikisha akila mdau wa burudani ambaye atafika siku hiyo anapata vionjo
vya kila aina ikiwemo wasanii mbali
mbali wa kizazi kipya ambao maskani yao ni Mkoa wa Pwani na wengine waalikwa
kutoka Dar es Salaam.
Kadhalika alisema kwamba kuanzishwa kwa eneo hilo la Kibaha
Carnival ni kutokana na wadau wengi wa burudani wanakosa sehemu ambayo ni
tulivu ya kwenda kutembelea katika siku za mapumziko hivyo kuzinduliwa sehemu
hiyo itakuwa ni mwanzo wa kuanzisha program mbali mbali za burudani na michezo
ili kuweza kukuza vipaji kwa wasanii wa kibaha na maeneo mengine ya jirani.
Katika hatua nyingine alisema kwamba kutakuwepo na viongozi
wa serikali katika sherehe hiyo ya uzinduzi rasmi ambapo pia kutakuwepo na
mashindano ya kula nyama choma ambapo washindi watajinyakulia zawadi kutoka kwa
uongozi wa Kibaha Carnival na kuongeza shghuli nzima hiyo itakuwa ikiongozwa na
Mc machachari hapa nchini Mc Jura pamoja na Scope V ‘mtoto wa kasuku.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.