ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 28, 2015

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA NAIBU WAZIRI ALIOWATEUA KUJAZA NAFASI ZILIZOSALIA, IKULU DAR LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha Prof. Jumanne Magembe kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, wakati wa hafla fupi ya kuwaapishwa Mawaziri wapya walioteuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Desemba 28, 2015. Picha na OMR
Mawaziri wapya walioteuliwa mwishoni mwa wiki wakisubiri kuapishwa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ikuli jijini Dar es Salaam,leo Desemba 28, 2015. Picha na OMR.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, kuwa Waziri wa Ujenzi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapishwa Mawaziri wapya walioteuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Desemba 28, 2015. Picha na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Dkt. Joyce Ndalichako (kulia) kuwa  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni  baada ya kumteua kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe.  Dkt. Philip Mpango (kulia) kuwa  Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua  kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Picha  na OMR
Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri waliohudhuri hafla hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri waliohudhuri hafla hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, na Makamu wake Mhe. Samia Suluhu Hassan, wakiwapongeza Mawaziri hao mara baada ya kuapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Desemba 28, 2015. Picha na OMR

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.